Ulimbukeni pia - kwa nini kiwe chuo kikuu cha chama badala ya chuo cha chama. Hii ni kupotosha na kubaka dhana nzima ya 'chuo kikuu'. Lakini iwapo kitapewa baraka na serikali, basi mkondo uwe huo huo kwa vyama vingine.
Taaluma ya uongozi inatolewa na vyuo vingi hapa nchini tangu enzi za Mzumbe, na wahitimu wamejaa mitaani. Kama lengo ni kuwapeleka wanafunzi wanaojua kusoma na kuandika( hata kuhesabu imeondolewa kama kigezo!) wapewe digrii, ni vema.