CCM imepotoka kuunda tume | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM imepotoka kuunda tume

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Netanyahu, Aug 23, 2009.

 1. Netanyahu

  Netanyahu Senior Member

  #1
  Aug 23, 2009
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Tume iliyoundwa na CCM kuchunguza mwenendo wa bunge sina imani nayo kabisa.

  Mjumbe Msekwa alibwagwa na kutolewa uspika na Samweli sitta hivyo kisasi chake atalipiza kwenye ripoti ya hiyo kamati kummaliza Sitta kwa kumkosesha kitumbua cha posho na umaarufu wa uspika.Ana kazi ya kuthibitisha umma kama atakalofanya na kutoa kwenye hiyo ripoti hana hasira na Sitta.

  Mjumbe Kinana alishatuhumiwa ufisadi huko nyuma na kuwa uraia wake ni wa mashaka inaelekea huyu mtu wa Kinana ambaye ni mtu wa Arusha kawekwa humo kuwakilisha maslahi ya mafisadi mmojawapo akiwa mtuhumiwa wa ufisadi wa Richmond kutoka kule Arusha kwa Jina ni Edward Ngoyayi Lowasa.Huyu Kinana ni part ya Arusha connection hivyo hawezi ya hawezi kumwangusha Lowasa atahakikisha anamlimba Sitta barabara kwenye hiyo ripoti uchwara ambayo ni uchwara hata kabla haijatoka.

  Mjumbe Mwinyi yeye ndiye baba mlezi kisiasa wa Kikwete.Ndiye aliyembeba kwenye mbeleko ya kisiasa hadi kumfikisha hapo alipo kwenye uraisi .Hivyo maadamu serikali ya mwaae kKikwete inashambuliwa vilivyo na bunge basi atamlinda mwanawe na kuhakikisha kuwa hiyo ripoti uchwara watakayotoa lazima imkandamize Spika na wabunge machachari.

  CCM ni chama kisicho na baba wa kisiasa.Toka afariki Nyerere watu walitarajia Labda Kingunge ndiye angekuwa baba wa taifa wa chama lakini upuuzi wa kupenda vihela umemharibu yule mzee hadi uwezo wake wa kujenga hoja za kisiasa umekufa.Mfano lilipoibuka suala la kadhi bungeni alikaa kinywa hakukemea lakini lilipokuja suala la waraka wa katoliki akaanza kuwaka na kuwa mkali akijifanya eti ghafla ni mkemeaji wa udini.La kadhi hadi leo hajalitolea tamko la kukemea mjadala wake ndani ya bunge na vikao vya chama.Angekemea mjadala wa kadhi bungeni na kwenye Vikao vya chama halafu akaja akakemea mjadala wa waraka wa katoliki angeibuka shujaa mkubwa kisiasa na kurudisha utukufu wake kisiasa uliopotea lakini wapi ndio maana wanamwona ni kibabu aliyefilisika kisiasa,kiitikadi na pia kimaadili ambaye hsikiliziki kisiasa tena.Akisimama kusema unajua amplifier ya mafisadi siyo ya wananchi imesimama kuongea.

  Mwinyi ameshindwa kupokea ubaba wa CCM sababu ya ulegevu na uswahili kwenye maamuzi mazito mahali pa kukemea hakemei anabaki tu yupo yupo tu labda hiyo kamati ajitahidi kufufuka aandike vitu ambavyo vitaonyesha kuwa yeye ni baba wa CCM na si wa Kikwete pekee pengine aweza ziba pengo,

  Ushauri wangu kwa wabunge ni kuwa mtu akisimama kuiponda serikali asibakize kitu amwage kila kitu.Kamati ya mwakyembe ingemaliza kila kitu kwenye Ripoti yake mafisadi wasingepata muda kujifanya kujisafisha na kuwasumbua.Nashauri kamati yoyote ya bunge ikiundwa au mbunge akipewa nafasi kuilimba serikali ahakikishe anailimba serikali barabara asibakize kitu chochote ndiyo dawa ya serikali maruhuni kama hii ya kikwete inayoendekeza mafisadi na kuendelea kuwatetea ndani ya chama na kusuka njama za kuwasafisha.
   
Loading...