Jamani ndugu zangu ccm imepatwa, au kwa maneno mengine ccm imepoteza tabia yake ya asili na uendeshaji wa mambo. Haijawahi kutokea katika chama cha viongozi wote kunyamaza na kuacha matamko yaendelee kuwa ndio sera na mpango mkakati wa maendeleo na dira ya chama kinachoongoza serikali. Sasa hivi hata katibu mkuu yupo kimya kiasi kwamba kuna jambo linaendelea, pia viongozi mbalimbali ndani ya chama tawala nikama wameshika tama,kiasi cha kushindwa pa kuanzia maana walizoe kabla ya matamko kutolewa lazima kuwepo na vikao na kujadili nini cha kutamkwa lakini siku hizi wanashituka na kupigwa butwaha kusikia matamko kwenye vyombo vya habari.
Ni nadra leo kuwaona viongozi waandamizi wa ccm wakiwa na tabasamu kwenye nyuso zao kama ilivyozoeleka. Je nini kimetokea au ccm imepatwa na nini?
Ni nadra leo kuwaona viongozi waandamizi wa ccm wakiwa na tabasamu kwenye nyuso zao kama ilivyozoeleka. Je nini kimetokea au ccm imepatwa na nini?