CCM imejifunika kichwa ili macho yasione wasiyotaka kuyaona

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,529
41,045
Ni jambo linalofikirisha sana, na kushangaza, na kuzua maswali mengi.

CCM inayafanya haya kwa nia ya kumdanganya nani? Au wanafanya kwaajili ya kumfariji nani?

1) CCM, kwa sababu zisizofahamika, imeamua kuacha kufanya kampeni za uchaguzi, na kugeuza mikutano iliyostahili kuwa ya kampeni, kuwa matamasha ya muziki

2) CCM, sijui ni kwa kujitoa ufahamu au dhamira ya kuamsha ghadhabu ya wapiga kura, kwenye matamasha hayo, mara kadhaa wametoa vitisho kwa wapiga kura kuwa wasipowachagua wagombea wa CCM, baada ya uchaguzi, watajuta. Hayo yalitamkwa na mgombea wa Urais kwenye tamasha la muziki lililofanyika wilayani Magu. Kila mwenye akili alibaki midomo wazi.

3) Kule Geita, kwenye matamasha hayo ya muziki, mgombea wa Urais wa CCM, aliwaambia wapiga kura kuwa wamchague yeye kwa sababu ni msukuma mwenzao. Je, ina maana tuiso wasukuma hatustahili kumchagua?.

4) Pale Mwanza, siku hiyo ya tamasha la CCM, shule zote, wakuu wa shule walielekezwa na Mkuu wa mkoa, kuwa siku hiyo kusiwe na masomo. Wanafunzi wote wapelekwe viwanja vya Furahisha kwenda kumsikiliza mgombea wa Urais wa CCM. Pia waliambiwa wasivae sare za shule. Pia walimu na watumishi wengine, wahakikishe wanahudhuria

5) Pale Mwanza, mgombea wa Urais kupitia CCM aliongea kidogo sana. Kisha akasema, sitaki niongee sana kwa sababu najua mmekuja kucheza muziki! Kwa hiyo hata yeye anajua wale watu waliokuwepo hawakuja kumsikiliza yeye bali walikuja kuangalia mauno ya wasanii.

Watanzania mwaka huu ni wa hasara. Watu wanaenda kwenye mikutano ya CCM ili wakasikie sera za CCM zenye kutoa matumaini katika kuwapa unafuu wa maisha kupitia ajira, ukuuaji wa uwekezaji, ongezeko la mapato yao, uhakika wa elimu na tiba bora, sera za makazi mazuri, kuondokana na watu wasiojulikana ambao kazi yao ni kuua, kuteka, kuwapoteza watu, na kupiga risasi watu wanaomkosoa Rais na Serikali; cha ajabu wanaoneshwa viuno vya wasanii!!!

Cha kujiuliza, wanafanya haya yote kwa lengo gani? Je, bila ya wanafunzi, bila ya kuigeuza mikutano ya kampeni kuwa matamasha ya muziki, wanaamini hakuna atakayekwenda kumsikiliza mgombea? Kama watu hawana hamu ya kwenda kumsikikiza mgombea, na kwenye kampeni wanafuata muziki, watakuwa na hamu ya kwenda kumpigia kura? Au siku ya uchaguzi wasanii watasambazwa vituo vyote vya kupigia kura kwa nia ya kuwavuta wapiga kura ambao kila wanapoenda hamu yao ni kuona viuno vya wasanii?

CCM, chagueni hata eneo moja tu ambalo mnaamini CCM inaungwa sana mkono, mfanye mkutano wa kampeni japo mmoja ili watu wasikie sera badala ya kuonesgwa wasanii. Msipeleke wasanii wala msilazimishe watu kuhudhuria bali mkiweza muwashawishi. Hiyo itawapa kipimo kizuri cha uungwaji mkono, na mtagundua kasoro zenu kuliko kujifunika kichwa ili tu msione msiyotaka kuyaona.
 
Wakikujibu majibu ya maana na yenye ushawishi niambie, niko hapa natapa kinywaji baada ya kazi ngumu. Maana ni nadra sana kwa wenye akili na hekima kusimama na kujidhalilisha kutetea chama cha hovyo kama hiki
 
Wapinzani kwa sasa wamekuwa watoa ushauri kwa CCM!

Yaani eti mtu anayetaka CCM ishindwe uchaguzi ndiye anayetoa ushauri ili CCM ishinde uchaguzi.

Kama kampeni za CCM ni matamasha, basi hii furaha kwenu wapinzani kwa sababu mnaenda kushinda uchaguzi!

Tanzania kuna vituko!

Inafurahisha kuwa Bado kuna wajinga wanadhani CCM itashindwa kwenye uchaguzi huu!
 
Kama ni matamasha ya mziki wee kinakuuma nini?? Na nyinyi tafuteni wasanii muwaweke... watanzania hawahitaji kusikia sera za ccm maana wameziona ndio maana tunasema mitano TENA nyie wengine ndio mtangaze sera zenu

CCM OYEEE
 
Wapinzani kwa sasa wamekuwa watoa ushauri kwa CCM!

Yaani eti mtu anayetaka CCM ishindwe uchaguzi ndiye anayetoa ushauri ili CCM ishinde uchaguzi.

Kama kampeni za CCM ni matamasha, basi hii furaha kwenu wapinzani kwa sababu mnaenda kushinda uchaguzi!

Tanzania kuna vituko!

Inafurahisha kuwa Bado kuna wajinga wanadhani CCM itashindwa kwenye uchaguzi huu!
Umeona ushauri tu? Hukuona maswali?

Nauliza tena, mgombea wa CCM aliwaambia watu wa Geita, wamchague kwa sababu yeye ni msukuma mwenzao, Je, tusio wasukuma haturuhusiwi kumchagua?

Yeye pia ni Rais wa nchi aliyekula kiapo cha kuwatumikia watu wote bila upendeleo.

Swali langu, kwa yeye kusema wasukuma wamchague yeye kwa sababu ni msukuma mwenzao, inamaanisha anawaelekeza watanzania wote wawachague wagombea wa makabila yao tu? Na makabila ambayo hayana mgombea wa kiti cha Urais anataka yasipige kura kwa sababu hakuna mgombea wa kabila lao?
 
Back
Top Bottom