R.B
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 6,296
- 2,573
MBUNGE wa Musoma Mjini, Vincent Nyerere (CHADEMA), amesema hakupoteza muda kufuatilia mkutano wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwani chama hicho kilishakufa baada ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kungatuka.
Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, Nyerere alisema CCM kwa sasa ni kikundi, kwani wao kwa wao wamebaki na siasa za kinafiki ikiwamo kuingia madarakani kwa kutumia fedha.
Alisema rushwa iliyokithiri katika chaguzi za chama, siasa chafu na kutotimiza ahadi walizotoa kwa wananchi kumeifanya CCM kupoteza hadhi ya awali iliyokuwa nayo enzi za Mwalimu Nyerere.
Aidha, aliiponda hotuba ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, na kusema kuwa wakulima wanataka vitendea kazi na si porojo zitolewazo kuhusiana na suala zima la kilimo.
Sioni Waziri Mkuu alichoongea kwani wakulima wanataka vitendo ambavyo ni vitendea kazi, wewe unamwambia mkulima kwa sasa tuweke mkazo katika suala la kilimo wakati humpi vifaa, ili atimize lile linalotakiwa, inasaidia nini? alihoji.
Nyerere alisema kuwa mkakati wa Kilimo Kwanza hauwezi kufanikiwa bila serikali kujipanga upya na kuwawezesha wakulima kuwa na vitendea kazi na elimu ya kutosha kufahamu suala zima la kilimo ili kiwe biashara kwao.
Akizungumzia suala la maendeleo katika jimbo lake, mbunge huyo alisema kuwa japo wanapokea fedha ndogo za maendeleo amejitahidi kuhakikisha anashirikiana na wananchi waliomchagua kuipatia maendeleo Musoma.