Sina mahusiano makubwa na siasa za CCM ila nimehakikishiwa kipande hiki kweli kimetokea. Cha ajabu ni kwamba maslahi ya Wananchi na kuliweka Taifa kwanza zinaitwa ni sera za Upinzani... Hapo mishipa ya akili imesimama, sijui niseme nini kuhusiana na CCM..
Ndio maana kila ninaposoma post za wateteaji ufisadi humu ndani kama anayejiita mkamap na wenzake, nazidi kupandishwa mori. Kelele na kejeli zao dhidi ya upinzani ndizo zinazidi kuchochea mwamko wa wananchi kutaka kutimua hili genge la wahuni (CCM) madarakani. Hivyo nawaomba waendeleze juhudi zao hizo za kubariki dhuluma kwa kuwa wanazidi kupalia mkaa wa moto hasira za wananchi. Kwa hilo nawapa pongezi Ladslaus na mkamap na wanaowaunga mkono.
Wewe ni dikteta wa fikra
Na dikteta wa namna hii ni mbaya kupindukia afadhali yule dikteta wa ki maumbo
Bado nakumbuka ulivyomtetea Mkapa bila kuyumba pamoja na hoja zote zilizotolewa humu ndani. Msimamo wako kweli ni wa kuigwa - maji ukiyavulia nguo bidi uyakoge. Kinachonitatanisha ni kukuelewa unasukmwa na nini, nani na kwa mantiki gani. Hizo zako ni mbinu kama za McCain dhidi ya Obama lakini yeye anasukumwa na ubaguzi, je wewe ?
Mkuu CCM ile unayozungmzia sio hii ya leo na kama mambo haya yangetokea wakati ule, tusingesubiri kina Dr. Slaa na Zitto. Huwezi kuitumia CCM ya mwalimu kutolea mifano ya Uongozi ambapo asilimia kubwa ya wachezaji wamekaa bench!..Ni sawa na kufananisha Yanga ya kina Sunday Manara na hii ya leo..Huwezi sema chadema ama SLAA ama ZITTO ndio kaanzisha hii move nenda nyuma kidogo uone nani alisababisha IDD SIMBA kujiuzulu,nani alisababisha Mbilinyi kama sikosei waziri wa fedha kujiuzulu na kwa sababu zipi?
Mkamap,
Mkuu CCM ile unayozungmzia sio hii ya leo na kama mambo haya yangetokea wakati ule, tusingesubiri kina Dr. Slaa na Zitto. Huwezi kuitumia CCM ya mwalimu kutolea mifano ya Uongozi ambapo asilimia kubwa ya wachezaji wamekaa bench!..Ni sawa na kufananisha Yanga ya kina Sunday Manara na hii ya leo..
Hata hivyo kina Idd Simba ulikuwa mchezo wa KULA ndani ya chama. Idd Simba alikuwa akijipanga kutafuta kura ndani na nje ya CCM ili kujiandaa na uchaguzi wa 2005. He did nothing wrong kiuchumi...
Mbinu ya sukari ilitumika kumwondoa kwani aliyeshiriki ktk mchezo mzima alikuwa mtu wa Rostam Aziz..kwa hiyo tunarudi nyuma tena kuwa hawa Mafisadi hawakuanza jana. Walianza ndani ya chama kiasi kwamba kina Dr. Slaa hawakuweza kuwaona hadi pale walipoanza kuonyesha makucha yao kitaifa..
Najitambulisha tena kuwa mimi sio mwanachama wa chama chochote bali mwananchi wa kawaida.ni nani alimuua chacha wangwe? kama kuna mkono wa mtu/watu hili halitajificha juu ya ardhi na mbingu! kwa kuwa imeandikwa kuwa damu ya abel nduguye itakulilia kila siku, na kamwe nitakuweka alama ili mtu asikuue!
Bado nakumbuka ulivyomtetea Mkapa bila kuyumba pamoja na hoja zote zilizotolewa humu ndani. Msimamo wako kweli ni wa kuigwa - maji ukiyavulia nguo bidi uyakoge. Kinachonitatanisha ni kukuelewa unasukmwa na nini, nani na kwa mantiki gani. Hizo zako ni mbinu kama za McCain dhidi ya Obama lakini yeye anasukumwa na ubaguzi, je wewe ?
Wewe ni dikteta wa fikra
Na dikteta wa namna hii ni mbaya kupindukia afadhali yule dikteta wa ki maumbo
1-Hivi nani alikuwa mtu wa mwisho kuzungumza na Wangwe pale Dodoma?
2-Hivi baada ya Chadema kumvua Umakamu, kifo cha Wangwe kilikua na athari gani kwa Chadema?
3-Je, CCM hawana "majasusi" wa kujua kwamba watu wanapogombana mmoja akivamiwa na majambazi, mtuhumiwa wa kwanza ni waliyegombana naye?
4-Hivi CCM walijiandaa ama hawakujiandaa katika kuhakikisha kifo cha Wangwe kinatumika kukibomoa Chadema?
5-Je, si ni kweli Chadema walishitukizwa katika propaganda kabla ya kuzinduka na kuanza kujipanga na kushinda uchaguz?
Kimsingi kukiwapo uchunguzi huru wahusika watatakiwa kutoa maelezo ya kwa mfano ilikuwaje CCM wakawa wamejiandaa na propaganda za kifo cha Wangwe hata kabla ya kifo chake, wachunguzi huru wanapaswa kuanza kuangalia mawasiliano na vikao vya mikakati.
Hapo watapata picha nani alijua kifo cha wangwe hata kabla ya kutokea na hapo wanaweza kujitetea kwamba waliambiwa na "Sheikh Yahaya" na hivyo kesi inafungwa na kuendelea na ile ya Deus Mallya kuendesha gari vibaya, vinginevyo mambo mazito yataibuka.