MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Yaani CCM wapewe tena ridhaa ya kuiongoza nchi hii kwa kipindi ambacho kwa sasa kila raia anapiga kelele na ugumu wa maisha! Gharama za vitu juu, pesa haipatikani kwenye mzunguko, kila kitu mambo yanalalamikiwa kutokwenda kama ilivyotarajiwa.
Sasa itokee CCM wapewe tena dola kwa kipindi ambacho atakayegombea hatarudi kupmba tena kuomba kura 2025 hali itakuaje? Raia tutakua na hali gani? Kwa sasa huenda kuna mambo yakarekebishwa kiasi ili kutengeneza kura 2020, lakini baada ya 2020 sijui hali itakuaje!
Mtakayemlalamikia hatarudi tena, kuna jamaa aliwahi kusema kuwa "hata msemeje sigombei tena" na hii ndio maana chama chake kilikuwa hati hati kuanguka na ndio maana kilinusurika.
Hii imekuwa ni hulka ya viongozi wengi hasa Afrika, mtu akishajua anaenda kumaliza muda wake haoni shida kuongoza atakavyo na ndio maana mrithi wake kwa kiasi kikubwa huja na Sera mpya. Vipi endapo CCM wakaongoza tena 2020?