Nicolas J Clinton Gabone
JF-Expert Member
- Mar 13, 2014
- 892
- 536
CHAMA CHA MAPINDUZI KIJISAHIHISHE
Comrades, tunakabiliwa na sura mpya na yenye mvutano mkubwa katika siasa za Tanzania. Muda mrefu migogoro ya kisiasa ilikuwa kati ya CCM na vyama vya upinzani. Lakini kwa sasa, hali imebadilika, mvutano mkubwa ni kati ya CCM na wananchi wenyewe. Jambo hili linaashiria mwanzo wa mabadiliko makubwa ya kifikra na kisiasa katika Taifa letu.
Maoni ya wananchi kwa viongozi wa serikali, ikiwemo mifano ya matamshi ya wazi yaliyojitokeza mbele ya Antony Mtaka, yanaonesha kuwa tatizo halionekani tena kuwa sehemu nyingine, bali ni CCM yenyewe. Chama kilichojikita kwenye misingi ya ukombozi kimekuwa sasa chanzo cha mgawanyiko, kutokana na maamuzi na vitendo vinavyolinda maslahi ya wachache ndani ya mfumo, huku wengi wakiachwa bila kusikilizwa.
Kutokana na kupungua kwa uhalali wa kisiasa kwa CCM mbele ya wananchi, inaonekana chama kinachagua kulinda nafasi yake kwa kushinikiza vyombo vya sheria na demokrasia, kukandamiza wakosoaji wa serikali na kudhoofisha uwezo wa vyama vya upinzani. Ni wazi kwamba mfumo unaotegemea ufisadi wa kisheria na matumizi ya nguvu, badala ya uhalali wa kijamii, hauwezi kuhimili shinikizo la muda mrefu.
Kufungwa kwa viongozi wa juu wa CHADEMA kwa tuhuma nzito za ugaidi na uaini, huku chama kikizuiwa rasilimali na uhuru wa kisiasa, ni ishara ya utekelezaji wa mkakati mpana, kuweka mazingira magumu ambayo upinzani unakuwa dhaifu kabla ya uchaguzi wa baadae. Hii ni dalili ya Taifa linaloingia kwenye siasa za hofu na udikteta badala ya siasa za ushindani wa hoja.
Kadiri CCM inavyozidi kuminya wananchi nafasi ya kueleza maoni yao, ndivyo chama kinavyojizidishia ugumu wa kuendelea kuaminika. Endapo mwenendo huu hautarekebishwa na/au kama mapinduzi ya haraka ya uchumi na maendeleo ya watu havitaonekana kwa macho ndani ya muda mfupi, msingi wa uhalali wa chama utazidi kuyumba, mfumo wa vyama vingi utadhoofika na mpishano na mgawanyiko wa kijamii utaongezeka kwa kasi. Katika kipindi cha miaka 5–10 ijayo, hofu ya CCM kupoteza madaraka inaweza kuwa kubwa kuliko uwezo wa chama kujirekebisha na kujisahihisha.
Historia ya kisiasa duniani inatuthibitishia jambo moja muhimu, nguvu inaweza kuchelewesha mabadiliko, lakini haiwezi kuyazuia milele. Wananchi wanapotambua na kukataa dhuluma, mabadiliko ya kisiasa yanakuwa lazima ya kutokea na mara nyingi yanatokea kwa kasi ambayo watawala hawakuwa wameitarajia au kujiandaa.
CCM IJISAHIHISHE KAMA HAIJACHELEWA