GAMBA KUU LA UFISADI CCM IGUNGA (GWIJI ROSTAM AZIZ) KIPEKEE LITABANDULIWA TU NA

MBUNGE WA PAMOJA TOKA KAMBI YA UPINZANI NCHINI!!

Mama yangu, mbona kwa CCM miti yote yateleza kiasi hiki kwa kila wakitendacho??

Ni vema ikaeleweka kwa kila mtu kwamba anguko la Gwinji wa Ufisadi nchini, Rostam Aziz, ni USHINDI kwa wanaharakati wooote ndani na nje ya nchi.

Hakika baada ya kuteseka sana na maisha magumu balaa ulisbabishwa na mafisadi wachache nchini, vijana hili ni FUNDISHO TOSHA kwetu kutokufanya ajizi Tabora.

Ni kweli kabisa kwamba WALAZWAHOI tunalo jukumu la kipekee kabisa la kutoweshwa kwake kabisa katika ramani ya siasa za nchi yetu ni jukumu la kila mmoja wetu ili kujihakikishia kwamba taifa letu Tanzania LINAZALIWA upya bila kuchukuliwa MATEKA tena wa huyu mtu, chama chake na au maslahi za nchi za nje anazoonekana kuziwakilisha katika nchi yetu.

Ndio, nasema kwamba ni jukumu la kila mpiga kura nchini, mpenda haki, mwanaharakati, mwandishi wa habari na akina kabwela tunaolazwa hoi na vituko vya huyu baba, kuhakikisha kwamba JUHUDI ZA KUNG'OA UFISADI NA MIZIZI YAKE YOTE ni sharti ianzie Igunga na kuenea kila kona ya taifa hili.

Kwa mshangao wa kila mmoja wetu jinsi ambavyo CCM kisivyokua na USO WA AIBU JUU YA UFISADI WA ROSTAM AZIZ bila kufikishwa katika mahakama yoyote nchini sasa tena waanza kupanga kupeleka MAKAPI na kulilazimisha kinywani mwao wananchi wa Igunga baada ya kuchukuliwa mateka kwa miaka mingi kwa nguvu za fedha za ufisadi.

Angalieni; mbali na Februari Makama kuwa ni miongoni mwa wabunge maarufu kwa DOSARI DONDA DUGU kuwahi kupitishwa kupitia MLANGO WA NYUMA na kisha KUJISHANGALIA MWENYEWE JINSI GANI ALIVYOWEZA KUTUA mjengoni Dodoma, hivi kweli WAADILIFU wote ndio hivo wameadimika ndani ya Chama hiki kiasi hicho kiasi cha CCM kuanza kuwazia kutuma JAMBAZi WA kule BoT, Mwigulu Nchemba, kwenda Igunga kuongoza safu ya kupatika MBUNGE WA WANANCHI atakayechukua nafasi ya aliyekua MBUNGE TX MWAKILISHI wa Maslahi ya Uajemi nchini ambaye pia anasadikiwa kuwa ni GAMBA KUU la Chama Cha Mapinduzi???????

Sasa ndugu zangu, kwa kuzingatia busara za usemi wa siku nyingi kati yetu kuwa 'Mtoto wa Nyoka ni Nyoka, je safu ya uchaguzi mdogo Igunga itakapongozwa ama na hili Jambazi letu la BoT ambaye bado kajinunulia fursa ya kuvinjari ovyo tu mitaani badala ya kule Keko au tusema kwamba itaongozwa na 'MBUNGE BLACK-MARKET' wa NEC kama ambavyo alivyo huyu dogo Februari Makamba; Watanzania TUTEGEMEE kuzaliwa kwa Mbunge wa aina gani Igunga??

Je, lengo letu kama taifa kulibandua Gamba Kuu la CCM, Rostam Aziz kwa kuweka Mbunge wa Wananchi kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi ya kuchukuliwa MATEKA wa Uajemi utakua umekidhikika kweli hadi hapo???

Baada ya yote, kutokana na majumuisho ya hapo juu na mengine mengi watakayoandika wenzangu humu, sasa nadiriki kusema chonde waheshimiwa Dr Slaa, Mwana Anga wa ukweli Mhe Freeman Mbowe, Vijana wa ukweli Zitto Kabwe, Julius Mtatiro na John Mnyika, James Mbatia, Kamanda Gobless Lema (Katapila), Simba wa Vita Tundu Lissu, Mwenyekiti wetu BAVICHA, nawaombeni sana tena sana KUONYESHA MSHIKAMANO WA KI-UPIGANAJI kwa Maslahi yetu sisi Walazwa Hoi kwa kumpitisha Prof Ibrahim Haruna Lipumba kuchukua kiti hiki cha uwakilishi bungeni.

Kwa kusema ukweli ninayo imani kubwa sana kwamba hili linawezekana sana tu kwenu kama ambavyo na sisi Machalii Wapiga kura nchini tunavyoiombea dua hivi sasa.