Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 20,389
- 38,667
Kuna juhudi kubwa sana zinafanywa na CCM "kuiokoa" CHADEMA ili isipotee katika ramani ya siasa za Tanzania. Ni CCM waliopiga sana kelele CHADEMA walipomchukua Edward Lowassa kwamba ni mtu asiyefaa kuwa mgombea Urais kupitia CHADEMA, ni CCM iliyowaita waliojiunga CHADEMA makapi na oil chafu.
Katika mambo mengi sana ambayo CHADEMA "inakosea" ni CCM kwa "wema" wake inakuja kusaidia ili mambo hayo yasiidhuru CHADEMA. Kuna hoja inayotolewa na CCM kwamba CHADEMA wametelekeza hoja ya ufisadi, au pia kuna ile nyingine kwamba chama hicho kinapoteza muelekeo. Hata la Wema kusemwa kwamba atajiunga CHADEMA limeshawakera CCM kwamba Mlimbwende huyo atakichafua cha hicho!
Hivi CHADEMA kuwa dhaifu si ndiyo utaisadia CCM kutawala milele kama wenyewe wanavyohanikiza kwenye propaganda zao? CCM haioni kuwa kuombea uimara wa CHADEMA ni kosa kubwa sana la kiufundi. Kwa nini CCM wasiachane na CHADEMA kwani uimara wa chama chao ndiyo utakao wasaidia kwenye ulingo wa siasa wa nchi yetu!
Sielewi ni kwa nini CCM inapoteza muda wake kuzuia CHADEMA isijifie wakati wao wenyewe huwa wanakiita chama hicho ni cha kibaguzi, kikanda, cha wavuta bangi na wanywa viroba, wapenda vurugu, na wasio na dira?