VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
CCM ni chama kikongwe kuliko vyote Tanzania. Wakati vingine vikianzia 1992,CCM yetu imeanza mwaka 1977. Pia,kwa miaka yote tangu 1977,CCM imekuwa chama tawala. Tumekuwa mfano wa siasa na utawala Tanzania na kwingineko.
Wakati wa kuonesha demokrasia chamani ni huu. Kama inavyokuwa katika kuwapata wagombea wetu wa Urais na Ubunge,na Uenyekiti wa Taifa uwe hivyohivyo. Tarehe ya uchaguzi itangazwe na ratiba itolewe. Wanachama waalikwe kugombea Uenyekiti.
Ule utamaduni na desturi ya kukabidhiana badala ya kuchaguana uachwe. Kwanza,ni kinyume cha katiba. Katiba ya chama inataka Mwenyekiti wetu achaguliwe katika mkutano mkuu. Pili,kukabidhi ni kuminya demokrasia chamani. Mwenyekiti anapaswa agombee na kuchaguliwa. Asikabidhiwe kama chama cha kifamilia.
CCM ni jumuiya kubwa. Kila mwanachama awe na haki ya kuwa Mwenyekiti. Ni muda wetu kuonesha vyama vingine ukomavu wetu wa demokrasia chamani. Desturi na mila haziwezi kuizidi nguvu Katiba!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Geita)