Uchaguzi 2020 CCM hii haiwezi kujirekebisha kamwe, tarehe 28 Oktoba iondoke ili ijirekebishe

JET SALLI

JF-Expert Member
Dec 1, 2014
1,992
1,196
Watu wachache wanadhani CCM ya siku hizi huwa inasikia. Toka atoke Mwalimu Nyerere madarakani na baada ya kifo chake CCM huwa haisikii kamwe.

Azimio la Zanzibar ndilo lililoleta CCM isiyosikia na CCM yenye kuuza viwanda, na CCM isiyojali maskini na huuzungumzia umaskini nyakati za kampeni pekee, halafu leo viongozi wake wanajinasibu kuwa wataleta viwanda, wataondoa umaskini ilhali wao ndio waliogeuza viwanda kuwa magodauni au maghala ya kutunzia nafaka.

CCM hii badala ya kuleta maendeleo imeleta ubaguzi mkubwa nchini kwa ajili tu ya tamaa ya madaraka kwa kutumia gia zifuatazo:-

1. Udini

2. Ukanda

3. Ukabila

4. Vitisho kwamba tukichagua upinzani kutakuwa vita vitu vyote hivi havina mashiko na vimenyima Watanzania maendeleo na kuwaletea umaskini mkubwa wa kutisha ilhali familia za viongozi zikiishi maisha ya kifahari kupita kiasi.

Maswali ya msingi ya kujiuliza ndugu zangu Watanzania ni kwamba, hivi wanaoshangilia CCM wanapata wapi huduma zao za kijamii kama vile.

1. Wanapata wapi huduma ya Maji?

2. Wanatumia umeme wa chanzo gani?

3. Wanatibiwa katika hospitali za Serikali gani ambazo hazina tatizo la madawa?

4. Hivi kweli watoto wao wanasoma pamoja na watoto wa viongozi katika shule zetu?

5. Hivi wanaoshangilia CCM wanaamini kabisa kwamba shule wanazosoma watoto wao ni bora kabisa na zina viwango vya kuridhisha?

6. Wanaoshangilia CCM wanajua kwamba ELIMU yetu imechezewa kiasi ambacho watoto sasa hivi hawayajui mambo mengi ya msingi?

MABADILIKO NI LAZIMA. WATANZANIA HATUWEZI KUENDELEA KUCHAGUA WAPIGA DILI CCM NA SISI KAZI YETU IKABAKI ETI NI KUWASHANGILIA AWAMU HII, HAPANA!

CCM IPUMZIKE ILI IJIREKEBISHE NJE YA SYSTEM.
 
Back
Top Bottom