CCM Hakuna Magamba, Watanzania ndio magamba magumu.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Hakuna Magamba, Watanzania ndio magamba magumu....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Hossam, Oct 25, 2011.

 1. Hossam

  Hossam JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 2,367
  Likes Received: 246
  Trophy Points: 160
  Sasa nimeamini CCM ni chama kiadilifu tena chenye misingi ileile aliyoiacha muasisi wake Mwl Nyerere, ni chama chenye kuwajali wamanchi wake na ni chama chenye dira safi na chenye kuwatakia watanzania maisha bora, na sasa kinaongozwa na rais msikivu kabisa Dk JK (Udaktari wa Hisani).

  Watanzania ndio magamba kabisa na wajinga mno na hata humu JF magamba ni wengi mno. Kuna ushahidi kwamba Watanzania ndio magamba na sio CCM, hebu fikiria haya machache;
  1. Badala ya vyama pinzani kuhubiri elimu ya uraia na sera zao wanamaliza muda wao mwingi kuhubiri vitu wasiokuwa na uhakika navyo kama, Kagoda, Deep Green Finance, Meremeta na mengine, mara safari za JK, mara Waziri Sitta ni mbea, sasa kama mnayajua hayo kwa nini msichukue hatua? Ni kwa nini mnapoteza muda na nguvu zenu kuhubiri vitu ambavyo hamna uhakika navyo? Ndio maana CCM inasema nyie ni magamba na mnachochea uvunjifu wa amani yetu na utulivu aisee.
  2. Hebu ona Watanzania wazalendo walivyolisukuma gari la Mh Jairo siku alipoambiwa na Luhanjo kwamba yeye sio mwizi! Hebu ona wafanyakazi wa kwa mzee megawatti walivyoacha majukumu yao nyeti na kuambulia kumpa maua ya utakaso. Nakikia mama mmoja aliachika baada ya mumewe kumuona kwenye runinga akimshangilia Jairo na wakati wakiwa nyumbani mama huyo ni mgonvi ajabu.
  3. Lakini pia ona wasaliti wa TBC1 ile ya Mhando. Sio Mhando aliyependwa kinafki na wafanyakazi wote TBC1 kwamba kaboresha ulaji na hali ya hewa? Lakini vipi alipotoka nje ya maelekezo sahihi ya CCM alidumu? Kwa nini wafanyakazi hawakuambatana nae? Kwa nini hawakubwaga manyanga? Unafki mtupu!! Hata hawa wapinzani wakichukua nchi hii unadhani haya ma V8 watayaachia? Kila mmoja atataka lake...
  4. Fikiria tena yaliyotokea kwa mtendaji mkuu wa TANROADS!! Vipi jamaa anamtunishia misuli hadi president, unayajua hayo? Nani aliumia na kwa uzalendo akashinikiza mkurugenzi huyo aondoke? Je huo sio umagamba? Ama wenzangu tafsiri ya magamba mnadhani ni wizi wa pesa sa umma? Hapana huo ni wizi sio magamba. Magamba ni wanafki na wanaovuruga mwenendo wa sera ila sio wezi ndio maana nasema Watanzania ni magamba magumu na akili zao zimeota kutu.
  5. Wanaharakati wamesema weee, waandishi wameandika wee hadi wengine kumwagiwa tindikali machoni, ni nani anawaelewa? Watanzania wako bize hawana muda wa kujua hatma ya maisha yao.
  Mungu atakuja kutuuliza haivi hizi akili alizotupa tulizitumiaje? Wengi watasema walizitumia kuendesha magari bila kugonga pindi monde ikiwa kichwani!!!
   
 2. R

  Real Masai Senior Member

  #2
  Oct 25, 2011
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nauliza kwani mwenye dhamana na nchi yetu c chama husika chenye kutenda kwa niaba yetu sisi watz..inakuaje sie ndio magamba...Halafu mdau hapo inavyoonekana shule yako haijakusaidia..nikiaanza na wewe na SISIEMU ndio mangamba na sio watz..angalia mwongozo na kauli ya mwisho ya uongozi wa nchi inatoka kwa chama tawala ndiyo inayotakiwa kutekeleza ilani ya chama kwa kutekeleza malengo waliojiwekea kwa wananchi wake...Nafkiri hebu rudi tena shule...
   
Loading...