CCM haiwezi kukaa siku 18, 615 bila kusinzia

CCM haiwezi kukaa siku 18, 615 bila kusinzia

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
17,985
Reaction score
17,380
Historia: Watu wenye mawazo mbadala na TANU/CCM walikuwepo kabla, wakati na hata baada ya Uhuru lakini walikuwa wanaoneka kuwa hawana maadili ndani ya CCM. Akina Zuberi Mtemvu, Oscar Kambona, Abdraham Babu, na kundi la wabunge 55 (G55) ni miongoni mwa watanzania hao ambao mawazo yao mbadala yalizimwa kihuni na TANU/CCM na kuonekana kuwa hawana maadili ndani ya chama, na kwa bahati mbaya hakukuwa na chama kingine ambako wangeweza kujiunga nacho zama zile za chama kimoja.

Vyama vingi: Hata baada ya kuanzishwa kwa vyama vingi nchini CCM iliendelea na ulevi wake uleule wa kuwaita watu wenye mawazo mbadala kuwa hawana maadili na wasiolitakia mema taifa.

CCM: Kwa mtazamo wa baadhi ya viongozi wakuu wa CCM ambao wengi wao tumezaliwa nao pamoja huko vijijini na kula, kukua, kucheza, na kusoma nao shule pamoja ghafla wanageuka kuwa wao ndio wenye uchungu zaidi na taifa hili kuliko watu wengine mara tu baada tunapowachagua kushika nafasi mbalimbali ndani ya chama na serikali. Watu hawa wanajifanya kuwa wanajua kila kitu watanzania wote wanachokipenda na wasichokipenda. Tabia yao hii imeendelea kuwa hivyo kwa miaka 51 takribani siku 18,615 za uhuru. Hadi hivi leo tunavyozungumza bado wao ndo wanaofahamu nani ana maadili na nani hana, nani ndo anafaa kuwaongoza watanzania na Tanzania. Na wakati mwingine huwa wanageuka watu hatari sana kwa watu wanaokwenda kinyume na wanavyofikiri na wanavyotaka wao iwe.

UKAWA
: ni vuguvugu ambalo chanzo chake halisi sio katiba ya Warioba, bali hawa ni watu walioshindwa kupata nafasi ya kutoa mawazo yao tangu kabla, wakati na baada ya uhuru wa nchi hii. Watu hawa kwa vipindi tofauti waliwatumia bila mafanikio watu kama vile akina Oscar Kambona, Abdrahamani Babu, Abood Jumbe, Maalim Seif, Njeru Kasaka, Christopher Mtikila, Lyatonga Mrema, Prof. Lipumba, Mbowe, Dr. Slaa, Marando, Lamwai, n.k katika kupambana na kubadilisha fikira za CCM na watawala kuwa wao pekee ndio wanaojuwa nani anafaa kuongoza na namna gani Tanzania na watanzania wote wanapaswa kuongozwa. Watanzania baada ya kujaribu njia mbalimbali za kuiondoa CCM tangu kabla, wakati na baada ya uhuru na hata baada ya kuingia mfumo wa vyama vingi na kushindwa, wamegundua njia mpya kuwa kuunganisha nguvu zao dhidi ya CCM kwenye uchaguzi ndio njia sahihi ya kutimiza adhima yao. Hivyo UKAWA ni sababu tu ya adhima yao hii mpya, na sijui kama njia hii nayo itashindwa watakuja na njia gani nyingine, nzuri au mbaya zaidi? maana hawatakubali mtu yeyote asimamishe mpango wao huo hata kama ikipita karne. Ni vizuri CCM ikaweka mazingira mazuri kwa watu wote wenye mawazo mbadala ya namna ya kuiongoza nchi hii kuendelea kutumia njia hii hii ya sanduku la kura badala ya zile njia nyingine zinazoambatana na hasara kwa mali na maisha.

Lowassa: CCM walidhani kuwa watakuwa macho na makini kwa miaka yote 51 ya uhuru (siku 18,615) bila ya kufanya kosa (kusinzia) hata kidogo, safari hii walisinsia na kufanya kosa la kukata majina ya wagombea urais wao bila kufuata utaratibu wa Chama chao (usingizi). Ujio wa mh. Lowassa UKAWA umeonekana kwa wapenda mabadiliko hawa sawa na mtu anayetaka kumpiga teke chura. Japo teke hilo linaweza kuwa na madhara fulani kwa chura mwenyewe lakini huwenda litamsogeza hatua kadhaa mbele kuelekea safari yake. Watu wenye adhima ya kufanya mabadiliko hawakujali kama LOwassa ni mzee, ni fisadi au ni mgonjwa, tena itakuwa mbaya zaidi kama maneno kama haya yatasemwa na CCM. Lowassa kwao wanamuona kama nyenzo muhimu, mzoefu, mwenye hela, mwenye watu, na mwenye mbinu mpya zaidi ya kushinda. Wako tayari kumfia ikibidi.

Lipumba na Slaa: Sio Lipumba, Slaa wala Zitto tu bali hata akiondoka nani UKAWA bado ukawa itabaki imara chini ya wale watakaobaki hata kama hawana sifa kubwa za uprofesa. Hivyo CCM isihangaike sana na viongozi wa UKAWA waliopo sasa watapoteza muda wao, maana wapenda mageuzi hawa walishajifunza kwa kilichotokea kwa akina Abood Jumbe, Lyatonga Mrema, Tambwe Hizza, Abbas Mtemvu, Masumbuko Lamwai, Mtikila, n.k walivyovuruga harakati zao mara baada ya kujitoa ghafla kwenye harakati zao kwa sababu wanazozijuwa wao. Safari hii hawatakubali tena kuona kiongozi wao mmoja awe chanzo cha kuvuruga harakati zao walizozianza kabla na baada ya uhuru. Bahati mbaya tayari kundi hili linafahamu kuwa viongozi wao ni walengwa wakuu wa majaribu mbalimbali.
 
Mkuu umesomeka na kueleweka vile vile.
 
Ninaimani Dk. Slaa bado tupo pamoja naye, atarudi kundini soon. Lipumba ndo kwanza amechochea moto wa Ukawa.
 
Tena UKAWA tutashinda kwa AMANI bila machafuko yoyote.....TUNATAKA TANZANIA YENYE TASWIRA YA MATUMAINI YA KWELI.
 
Saa saba mchana tu rais wetu lowassa atakuwa ameshatangazwa!!
 
11880462_1457722734533868_928390379812071348_n.jpg
 
masikini rasi wetu wa mioyoni'' mbowe wewe ni mubayaa! yaani umemtosa rais wetu wa moyoni!
ulituaminisha kuwa 2010 alishinda kumbe ulikuwa unatuhadaa. na sasa umedhirisha kuwa hakushinda na wala asingeshida. ama kweli mbowe wewe ni mubaya. masiki rais wetu wa mioyo!
 
kavulata uneonyesha uwezo binafsi kiuchambuzi.hakika tread zenye uchambuzi wa kina ndizo zinazohitajika kwa wana JF
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom