salisalum
JF-Expert Member
- Oct 27, 2010
- 434
- 159
Tangu nianze kupiga kura wakati wa chama kimoja hadi leo sijawahi kuona uchaguzi kama wa mwaka huu. Uchaguzi wa kihuni na uhuni huo unafanywa waziwazi.
Watanzania inabidi ifike mahali tuseme sasa basi. Bora watawale wakijua hawana mandate ya Watanzania. Tuwakatae. Hakuna mtu wa kutulazimisha kupiga kura, tuwakatae. Huu siyo uhuni tu ni ushenzi na ubedui usiomithilika katika enzi hizi za ustaarabu.
Watanzania tunawaachia miaka mitano watawale, wakusanye kodi, waibe, wafanye kila kitu. Sisi tuna siku moja tu ya kuamua, siku moja tu nayo wanaipoka. Zoezi simple la kuamua tunataka nchi iongozwe na nani miaka mitano ijayo linatungiwa sheria na kanuni mamia ya kurasa za ukubwa wa A4! Mamia ya kurasa. Mara ukipiga kura ukae mita 200, mara nakala ya matokeo itatolewa kwa mawakala kama kuna nakala za kutosha, mara mawakaka wasiingie na simu, ili iweje?
Iweje kupiga kura unanitongoza lakini mara tu nikipiga nakuwa adui wa kituo cha kupigia kura? Sitakiwi hata kuona matokeo ya kura yangu? Sheria za kijinga kabisa. Hivi kama makazi yako karibu na kituo, baada kupiga kura nihame? Sasa wanaseme ukipiga kura rudi nyumbani ukalale, unanipangiaje ratiba yangu?
CCM wanapita kukusanya shahada/vitambulisho vya kupigia kura, ili iweje? Baadhi ya wapiga kura wamelalamikia jambo hili. Matendo haya ni jinai lakini yanafanywa na CCM.
Mnaotaka kupiga kura katika mazingira haya tafakarini sana.