Ccm hadi kwenye treni????

Ccm hadi kwenye treni????

Doppelganger

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
1,858
Reaction score
758
habarini wana JF.
Ni wazi tunatambua kuwa CCM ni wavurugaji na wavurundaji wa mambo,na kwa jinsi siku sinavyozidi kwenda wanazidi kuweka bongo zao pembeni na kufanya watakavyo.

Hii nimejuzwa muda huu;

Treni iliyotarajiwa kuondoka Kigoma kuelekea Dar es salaam leo saa Kumi alasiri,inatarajiwa kuondoka majira ya saa mbili na saa tatu usiku wa leo ili kuwasubiri wanachama wa CCM wanaosherehekea maadhimisho ya miaka 36 ya Chama chao.

Kwa mujibu chanzo kilichopo stesheni ya Kigoma,hata mabehewa yanayotarajiwa kutumika kwa safari hayajapangwa hapo stesheni ili kuepusha malalamiko ya wasafiri walio tayari kwa safari na pia kuwapa kuwapa muda wa kutosha wanaCCM kusherehekea na kujiandaa kwa safari.
Chanzo hicho kinajuza kuwa amri ya kubadili ratiba hiyo ya treni ilitolewa tangu asubuhi lakini uongozi haukuwatangazia wasafiri ili kuepusha maswali yasiyo na majibu.

Hivi kwanini CCM wasiliite shirika la reli kwa jina lao ili ijulikane wazi kuwa ni lao?
Kwanini CCM wanashindwa kuwa wastaarabu na kujua kuwa wapo wasafiri wanaowahi matibabu,biashara,n.k kwa usafiri huo ambao unaonekana kuwa wengi wanaumudu?
 
Watafanyeje sasa wakati nan amewanyima basi zake, yule wa pale Kwa shabiby bus....! wenyewe wanazuga wameamua wenyewe!
 
so long wanalipa nauli sioni shida. kwani hiyo train haijiendeshi kibiashara? kwa nini waache abiria? au wewe hujawahi kupanda daladala halafu kundi la abiria likatoka, utalalamika lakini konda hatakuwa na time na wewe. tumia akili kidogo kufikiria.
 
Back
Top Bottom