CCM fungueni macho

Sijapata nafasi ya kusafiri kwenda mikoa ya kusini naagharibi lakini huku Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Singida, Tabora, Shinyanga, Mwanza, Kagera ni 90% UKAWA! Kila mtu ni Lowasa ndo rais
 
Kufanananisha uchaguzi wamwaka huu na 1995 enzi ya Mrema nikujidanganya.

Ikumbukwe 1995 ulikuwa niuchaguzi wakwanza kwamfumo wavyama vingi natulikuwa ndokwanza tunamiaka mitatu tangu mfumo huo uanze. Kwa waliokuwepo watakumbuka matangazo mbalimbali yakuwahadaa wapigakura kwamba wakichagua wapinzani watasababisha vita. Watu waliowengi waliyaamini matangazo hayo nakwa kiasi flani inawezakuwa ilichangia kumpunguzia mrema kura. Tujiulize kwa watanzania waleo walioshuhudia makeke mbalimbali yawapinzani kama kina Tundu lisu, John Mnyika, Peter Msigwa, Mr.Sugu, David Kafulila nk, ninani wakuambiwa wapinzani wataleta vita akaamini? Jibu ni0.

Vilevile 1995 mtu aliyefanyakazi kubwa kubadili upepo alikuwa baba wa Taifa. Alikuwa ndomtu pekee ambaye watanzania tulimuamini kutokana nautumishi wake uliotukuka. Mwalimu hakutuibia, alituongoza kwa weledi mkubwa. Mungu amlaze mahala pema baba wawatu. Leo tujiulize nikiongozi gani mstaafu atatueleza lolote watanzania tumuelewe? Hakuna hatammoja wote niwezi nawanafiki wakubwa.

Mfano tumeshuhudia kashfa mbalimbali zakuliumiza taifa, nahao wastaafu wapo. Hatujawahi kuskia sauti zao wakikemea popote. Ila Mwl angekuwepo tunaimani walahata kutokea hizo kashfa zisingetokea. Au zingetokea angetoka Butiama hata kwamguu endapo wangemnyima usafiri.

Kwahiyo huu moto wamwaka huu umeshawaka nahakuna wakuuzima. Hilo likowazi kwamtu mwenye kufuatilia hali yamambo utajua tu.
 

Very well said Makele mbele
 
Last edited by a moderator:
Mlachake yaani maswali uliojiuliza nami najiuliza hivyo hivyo....katika watu woote nliokuwa nao karibu, ni kama watu 6 tu ndio CCM, sasa huo ushindi unatoka wapi??
 
Last edited by a moderator:

Mwenye masikio na asikie. Ameni
 
Baada ya trh 25 ndo utapata majibu ya wa Tz. Hata mrema alihesabu hivyo hivyo lakin kapet la ikulu hakuliona.

unamsemea mrema wa 1995?amka wewe na toa tongotongo zako kwa maji ya moto. ...
 
Poa lakin siasa ni game lisiloeleweka kwa wananchi. Unaweza ishia kulia machozi. Wa Tz ni wale wale na siasa ni ile ile. Subiri kipenga.
 
jamani mm nko tayar kubet, LOWASA anashinda..
anayepinga aje tubet#…
 
Mungu kaamua kuwafunga macho ccm.ukawa hoyeeee lowasa mungu yupo nawe urais huuuuuuuoooooo
 
Nimeshangaa hata mke wangu kumbe UKAWA pamoja na kuwa busy hata kufuatilia taarifa za habari.
 
Mimi nasubiri stori za kuibiwa kura na kuporwa ushindi hapo baadae
 
Mimi nimeshangaa familia yangu yote Ukawa, Shuleni ninakofundisha wanafunzi 18 yrs + 90% Ukawa. ccm hawatoki.
 
Kama aliyosema Kubenea kuhusu BVR ni kweli basi Lolote laweza tokea Ufanisi wa NEC ndiyo suluhu.Muda wa kampeni bado upepo waweza badilika
 
Ukawa ni watu wa kujionyesha, wabishi makelele tuuu, sasa ccm weng saiv wamejua ukitaka kubishana nao wanakua kimya ila kwenye sanduku ndo mpango mzima, maana unaweza umiza mishipa ya taya kujibishana nao. Sasa kule ndo kiboko ya wote. MAGUFULI FOR CHANGE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…