CCM: "Every generation needs a new revolution" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM: "Every generation needs a new revolution"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mr Emmy, Apr 3, 2012.

 1. M

  Mr Emmy JF-Expert Member

  #1
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 1,201
  Likes Received: 289
  Trophy Points: 180
  Kwanza napenda kutoa pole kwa wana CCM wenzangu kwa kupoteza jimbo letu la Arumeru Mashariki na pia Nakipongeza Chadema kwa ushindi mwembamba walioupata katika jimbo la Arumeru na pia na mpongeza J. Nasari kwa kupewa ridhaa na Wana Arumeru kuwa Mbunge wao ila namatahadharisha 2015 sio mbali kwana CCM tunakwenda kurudisha jimbo letu tulilolipoteza siku ya tarehe 1/04/2012.

  Kwa wana CCM wenzangu tunatakiwa kutambua sasa kuwa kila kizazi kinahitaji mapinduzi yake mapya hivyo basi tujipange kuanzisha vuguvugu la mapinduzi mapya kwa kizazi cha sasa ili tuweze kujiamarisha na kuendelea kukubalika kwa wananchi wote wa Tanzania. Kila mapinduzi yana gharama yake tusiogope kufanya maumuzi magumu kwa manufaa ya kizazi kipya cha watanzania na kwa manufaa ya chama.

  Wahenga walishasema "Only the wisest and stupidest of men never change." and "Change is the law of life and those who look only to the past or present are certain to miss the future." Wana CCM wenzangu ni muda muafaka wa kubadilika na kuleta mapinduzi mapya katika chama chetu kwa manufaa ya watanzania na wapumbafu wachache wasiokuwa na busara wanatakiwa kutoswa baharini, I mean kuvuliwa uwanachama na kuchukuliwa hatua stahiki.

  Naipenda sana CCM yangu cjaona mbadala zaidi yako ila naona wanafiki na wazandiki ndani ya ccm wanaokusaliti na kuwapa nguvu genge la wahuni linatumia vibaya sauti ya Watu hasa vijana kujipatia nguvu, madaraka na matumaini ya kuitawala Tanzania. Sasa muda umefika wa kufanya Mapinduzi mapya kwa kizazi kipya kupitia CCM Mpya

  [h=2]The future of our country belongs to CCM new generation and revulution tuungane pamoja kujenga Taifa letu kupitia CCM mpya.[/h]

   
 2. m

  mharakati JF-Expert Member

  #2
  Apr 3, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  unaonekana ni mkereketwa mzuri tu wa chama chako siyo siri CHAMA CHA MAPINDUZI KINAHITAJI MAPINDUZI ili kipate tena ridhaa ya wananchi wa tz kuongoza kwa miaka michache iajyo.

  Pamoja na kwamba kushindwa kwa CCM huko Arumeru siyo kitu cha kushtua kutokana na jimbo kuonekana lilikua karibu zaidi na ngome ya upinzani kuliko kuwa CCM (kata zote kando ya barabara ya Moshi-Arusha toka KIA hadi Arusha mjini ni za CDM na siyo CCM) bado CCM inabidi ifanye tathmini ya kina kuonyesha kuwa imekua mbali na siasa za upinzani zenye sera na siyo vijembe, matusi na ujinga mwingine ulioongelewa na makada mbali mbali wa CCM.. Ikiwa demokrasia ni soko huria na kila mwenye bidhaa anajitahidi kuiboresha ili iuzike basi bidhaa ya CCM (angalau katika chaguzi hii ndogo) ilikua ni hafifu na imepitwa na wakati na ilistahili kutonunuliwa na wananchi.

  Wana CCM wanamatatizo mengi yakiwemo makundi hasimu ndani ya chama, serikali kutojali wananchi na kuzidi kwa kero za kijamii na kiuchumi, kudidimia kwa demokrasia ndani ya CCM na haswa mfumo wa kuwapata wagombea wake wa viti mbali mbali, na kusahau wanachama wake wa kawaida kwa kutojali maslahi ya wengi na kukumbatia matajiri wachache..

  kwangu mimi makundi siyo tatizo kwani hata vyama vikubwa duniani vina makundi yanayopingana kiitikadi za ndani na kimaslahi fulani fulani ili linaweza tatuliwa kukiwa na mwenyeketi msikivu, mwenye kusikiliza wananchama walio wengi na mwenye asiye muoga mwenye kuoanisha maslahi ya chama na yale ya kitaifa..kwa sasa JK siyo mtu huyu na hii ni shida kubwa makundi yanakua hayadhibitiki.

  CCM inahitaji kitu kimoja kikubwa nacho ni kuoanisha maslahi ya taifa na yale ya chama ili kuzalisha serikali bora, kuchagua makada jasiri, wazalendo na wasiowekwa na wachache kwa manufaa ya hao wachache, kuongeza demokrasia ndani ya chama na uwazi katika kuwapata wagombea wake kulingana na matakwa ya wanachama walio wengi na wananchi kwa ujumla..hii itamapa mwenyeketi na sekreatariet yake nguvu katika kusimamia maslahi ya chama na kuwawajibisha wale wote wanakiuka maadili ya uongozi katika chama na serikali yake. hii itawapa nguvu katika majukwaa ya kisiasa na kutoaibishwa kwa sababu watakua wanajua wanaenda kutekeleza agenda ya wananchi na hawatakua na tuhuma nyingi za kujibu.

  CCM ya namna hii haitokua kichaka cha waovu na wabadhirifu na wezi wa mali zetu za umma, CCM ya namna hii itakua inafuata misingi yake halisi na itrikadi yake ya wakaulima na wafanyakazi, CCM ya namna hii itakua inaoana na historia yake ya ukombozi wa taifa hili, CCM ya namna hii italeta maendeleo na itadumu milele
   
 3. M

  Mzee Kipara Member

  #3
  Apr 3, 2012
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 83
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 15

  Hivi kati ya CCM na CDM nani ni genge la wahuni? Wewe upo nchi hii kweli? Maana nashindwa kuamini kama huoni maouvu, unyama, wizi, oungo, matusi na mabaya mengine mengi ambayo CCM wanafanya. Usiruhusu upenzi wa chama ukapitiliza mpaka kukuziba macho.
   
 4. nashy

  nashy JF-Expert Member

  #4
  Apr 3, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 679
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Emmy nadhani ni sawa na kibajaji
   
 5. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #5
  Apr 3, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Simple Logic ... "Genge la wahuni"

  Limewezaje kulizidi hilo genge la CCM ... Wahuni wawashinde CCM ..then Who are You REAL?? Better than Wahuni or Much worse ... and if that is the Case who are you SIR? Songa mbele jibu swali!!!
   
 6. M

  Mr Emmy JF-Expert Member

  #6
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 1,201
  Likes Received: 289
  Trophy Points: 180
  kama umesoma viziri nimeainisha mapungufu yaliyopo CCM nakusema CCM inahitaji mabaliko kwanza ili kuliokoa Taifa kuangukia katika mikononi mwa magenge ya kihuni ambayo yanatumia udhaifu wa CCM sasa kujipatia umaarufu na uungwaji mkono kutoka kwa wananchi hasa vijana.
   
 7. M

  Mr Emmy JF-Expert Member

  #7
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 1,201
  Likes Received: 289
  Trophy Points: 180
  usiwe mvivu wa kusoma na kuchambua kwahiyo soma habari nzima then anzisha hoja ya msingi ambayo ninatakiwa kuijibu ama kujibiwa na wana CCM Mabadiliko
   
 8. v

  vngenge JF-Expert Member

  #8
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 366
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Una mawazo mazuri sana. Tatizo naona wenye chama chao hawako tayari kubeba hiyo gharama ya kufanya renovation kwa sababu hailipi kwao!. Chama hiki kimekuwa si cha wanyonge tena, kimekuwa si cha wafanyakazi na wakulima .Nikupe mfano wafanyakazi walipotaka kugoma kudai nyongeza ya mshahara walijibiwaje?, Kima cha chini cha mshahara laki na nusu kwa inflation hii unategemea mfanyakazi gani atakuwa na mapenz na hiki chama. Kodi ya chumba minimum 30elf, kwa kujibana ana vyumba vitatu kimoja mwenyewe kingine watoto wa kike na kingine watotot wa kiume, nauli chakula, umeme, maji hivi hiyo 60 iliyobaki inatosha? leo hii umuambie piga kura cccm ikupe maendeleo atakuelewa? huku huyo anaetakiwa kumpigia kura anajadili posho ya laki 2 kwa cku jamani mbona hesabu rahisi sana!. Ishu ya madaktari badala ya kufikia mutual agreement ubabe unatumika na hawa ndio wapo karibu na wapigakura je watatoa huduma kwa kujituma? Bado malalamiko ni mengi sana na hali ya maisha ni ngumu. Hamna ubunifu tena kwa watendaji umebaki uzoefu tu kitu ambacho kasi ya mabadiliko ya kisayansi, teknoloji, uchumi, masoko na mifumo ya kiuzalishaji haitegemei mazoea bali tafiti za kisayansi na ubunifu wa mikakati endelevu. Sisa hii watendaji wengi wazee hawana wamebaki kuongeza kodi bidhaa zilezile bila kujali athari kwa mlaji wa mwisho. Hii ni hatari na tutegemee zaidi ya haya siku za usoni. Wakati wenzetu wanasugua vichwa namna gani watakuza uchumi from micro to macro economy sisi tumeng'ang'ana chama flani wadogo kama kokoto, sijui nani sio mtoto wa nani...ooh na sijui nali alifukuzwa upadre umeacha ofisi ya umma, unatumia muda wa umma mafuta ya umma wakati wings za chama zipo. Wazir unaacha ofis kwenda kwenye kampen hii inaonesha namna gani msivyojiamini. KLOROQUIN NI CHUNGU LKN NDIO DAWA, CHAGUENI KUBADILIKA AU KUANGUKA KWA KISHINDO.
   
Loading...