CCM Dodoma Mjini Yawafikia Mabalozi 2242 Kuwaandaa na Uchaguzi wa Tarehe 27.11.2024

CCM Dodoma Mjini Yawafikia Mabalozi 2242 Kuwaandaa na Uchaguzi wa Tarehe 27.11.2024

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,428

CCM DODOMA MJINI YAWAFIKIA MABALOZI 2242 KUWAANDAA NA UCHAGUZI WA TAREHE 27.11.2024

Uongozi wa CCm Wilaya ya Dodoma leo umekamilisha kuwafikia idadi ya Mabalozi wote 2242 wa Jimbo la Dodoma Mjini lenye kata 41 na mitaa 223 kwa kukutana na mabalozi wa Tarafa ya Zuzu kutoka Kata za Chigongwe, Nala, Mbalawala, Mbambala, Zuzu, Matumbulu na Mpunguzi.

Mikutano hii ni mfululizo wa mikutano inayoongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya Cde. Charles Mamba ya kukutana na mabalozi wote wa Dodoma Mjini kwa lengo la kuwajengea uwezo na kutoa hamasa ya wanaCCM kushiriki kwa wingi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.

“Tumezungumza pamoja na kuelewana vizuri na mabalozi wetu,na wapo tayari kukamilisha ushindi wa kishindo wa CCM.

Hili ndio Jesho kubwa la CCM tukutane Tarehe 27.11.2024 kwenye uchaguzi ambao naamini CCM itafanya vizuri sana kwa kuwa tumejipanga na kujiandaa vizuri“Alisema Mamba

Naye Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde amewapongeza mabalozi kwa kazi nzuri ya hamasha wakati wa kujiandikisha kwenye daftari la mkazi na kuwaomba kufanya vizuri zaidi kuhamasisha watu wajitokeze na kuichagua CCM.

Katibi wa CCM wilaya ya Dodoma Mjini Ndg. Sofia Kibaba amewataka mabalozi wote kuzingatia taratibu zote za uchaguzi na kuhakikisha wanaongoza ubalozi wao kupiga kura mapema kabisa.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-11-25 at 16.50.59.jpeg
    WhatsApp Image 2024-11-25 at 16.50.59.jpeg
    75.7 KB · Views: 13
  • WhatsApp Image 2024-11-25 at 16.50.59 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-11-25 at 16.50.59 (1).jpeg
    77.4 KB · Views: 19
  • WhatsApp Image 2024-11-25 at 16.51.00.jpeg
    WhatsApp Image 2024-11-25 at 16.51.00.jpeg
    92.3 KB · Views: 21
  • WhatsApp Image 2024-11-25 at 16.51.00 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-11-25 at 16.51.00 (1).jpeg
    115.2 KB · Views: 22
  • WhatsApp Image 2024-11-25 at 16.51.01.jpeg
    WhatsApp Image 2024-11-25 at 16.51.01.jpeg
    110.4 KB · Views: 19
  • WhatsApp Image 2024-11-25 at 16.51.01 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-11-25 at 16.51.01 (1).jpeg
    97.9 KB · Views: 21
  • WhatsApp Image 2024-11-25 at 16.51.02.jpeg
    WhatsApp Image 2024-11-25 at 16.51.02.jpeg
    124.8 KB · Views: 19
  • WhatsApp Image 2024-11-25 at 16.51.02 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-11-25 at 16.51.02 (1).jpeg
    128.8 KB · Views: 18
  • WhatsApp Image 2024-11-25 at 16.51.03.jpeg
    WhatsApp Image 2024-11-25 at 16.51.03.jpeg
    75.4 KB · Views: 17
  • WhatsApp Image 2024-11-25 at 16.51.04.jpeg
    WhatsApp Image 2024-11-25 at 16.51.04.jpeg
    55.8 KB · Views: 20
Back
Top Bottom