CCM Dar wamlilia Kinana maisha magumu

Sumasuma

JF-Expert Member
Jun 23, 2011
342
110
Keneth Goliama na Shakila Nyerere
ALIYEKUWA Meneja kampeni wa Rais Jakaya Kikwete katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, Abdulrahaman Kinana amejikuta katika wakati mgumu katika ziara yake ya kutembelea Ofisi za CCM Mkoa wa Dar es Salaam baada ya kutakiwa kufikisha salamu kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete kwamba maisha yamekuwa magumu.


Kuanzia Januari 25 mwaka huu, Kinana alianza ziara yake kutembelea matawi mbalimbali ya CCM mkoa huo ambapo pia alisikiliza kero za wananchi na wanachama wa chama hicho, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 35 ya kuzaliwa kwa chama hicho ambayo kilele chake kilikuwa juzi jijini Mwanza.

Akiwa katika ziara hiyo na kuhitimisha eneo la Buguruni juzi, Kinana alikabiliwa na swali kuu kuhusu hali ngumu ya uchumi inayowakabili wananchi ukiwamo mfumuko wa bei huku wakimwambia yeye ndiye aliyemnadi Rais Kikwete.

Kinana mwenyewe akifafanua zaidi alisema, "Kuwa kampeni meneja ndiyo imekuwa nongwa, loo! Sawa basi nitamfikishia salaam Rais kwa sababu nina uwezo wa kufanya naye mawasiliano ya karibu tu."

Alisema kila alikopita na sehemu kubwa ya watu waliosimama kuulizwa maswali walijikita katika hali ngumu ya maisha, kitu ambacho aliahidi kukifikisha kwa Rais ili ajue jinsi umma unavyolalamikia makali ya maisha.

Alifafanua kwamba kutokana na malalamiko hayo ya ugumu wa maisha, ameona ni jambo zito ambalo linapaswa kufanyiwa kazi kwa haraka na ili kulifanikisha hilo aliona ni vema akawasiliana na Rais.

Alisema licha ya malalamiko yote hayo ya wananchi hajutii kumnadi Kikwete, lakini atahakikisha ahadi zote zilizotolewa wakati wa kampeni zinatekelezwa.

"Siwezi kujuta maana nilimnadi mimi na nitaendelea kumtetea. Huyu ni wangu hadi mwisho, lakini nitamfikishia nilichoambiwa na wananchi pamoja na kuhakikisha tunatekeleza ahadi zetu tulizotoa kwa wananchi," alisisitiza Kinana.
:A S 465:
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom