CCM chali Igunda - Kauli ya Dk. Slaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM chali Igunda - Kauli ya Dk. Slaa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sir.JAPHET, Aug 22, 2012.

 1. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #1
  Aug 22, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kauli ya Dk. Slaa
  Baada ya kutenguliwa kwa Ubunge wa Dk. Kafumu, Dk. Slaa alisema hukumu hiyo ni ya kihistoria kwa Tanzania na kwamba chama chake kimeweka historia nyingine katika siasa za Tanzania. Alisema kwamba, mambo yote ambayo walikuwa wakiueleza umma, kwamba CCm wanafanya makosa ya kugawa mahindi, zimeonekana ni za kw[h=2]CCM chali Igunda - Nape, Dk. Kafumu watoa kauli [/h]eli.[​IMG]Nape, Dk. Kafumu watoa kauli
  Muda mfupi baada ya hukumu kutolewa, Dk. Kafumu alinukuliwa katika Kituo cha Televisheni cha ITV, akisema anakiachia chama chake kitoe uamuzi.

  Alisema kwamba, hukumu hiyo imetolewa kwa upendeleo mkubwa, kwani mashahidi wake walikuwa wakitishwa na kuulizwa maswali kwa kufokewa.

  Katika hali ya kujifariji alisema yeye ni mtaalamu wa masuala ya madini na ataendelea kubaki na fani yake hiyo.

  Kwa upande wake, Nape alisema hawezi kuzungumzia hukumu hiyo kwa sasa hadi atakapopata taarifa ya CCM, kutoka mkoani Tabora.

  Habari hii imeandaliwa na Chuma Shomari, John Makambo, Abdalah Amir Nzega, Arodia Peter na Benjamin Masese, Dar.
   
 2. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #2
  Aug 22, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  [​IMG]Aliyekuwa mbunge wa Igunga, Dk. Peter Kafumu

  *Mahakama yamvua ubunge Dk. Kafumu, uchaguzi haukuwa huru na haki
  *Chadema wafurika mahakamani, vigogo CCM wamtelekeza Dk. Kafumu
  *Dk. Slaa asema ni hukumu ya kihistoria, Rage chupuchupu kwenda jela
  MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Kanda ya Tabora, imetengua matokeo ya ubunge wa Mbunge wa Igunga, Dk. Peter Kafumu (CCM).

  Hukumu hiyo ilitolewa jana na Jaji wa Mahakama hiyo, Mary Shangali kutokana na kile alichosema kuwa, uchaguzi uliompa ushindi Dk. Kafumu ulitawaliwa na vitendo vya rushwa, kampeni chafu na vitisho dhidi ya wapiga kura.

  Jaji Shangali alitangaza kutengua matokeo hayo baada ya kuridhika na hoja saba zilizowasilishwa na upande wa mlalamikaji kati ya hoja 17 zilizowasilishwa mahakamani hapo.

  Kesi hiyo ilifunguliwa na Mlalamikaji aliyekuwa mgombea wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Joseph Kashindye ambaye wakati wa kesi hiyo, aliwakiwakilishwa na Wakili Maarufu nchini, Profesa Abdallah Safari akisaidiana na Gasper Mwanalyela wa jijini Mwanza.

  Katika shauri hilo, Kashindye ambaye ni mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, alikuwa akipinga matokeo ya uchaguzi huo yaliyompa ushindi Dk. Kafumu kwa kile alichodai kuwa, kulikuwa na ukiukwaji wa sheria na taratibu za uchaguzi huo.

  Upande wa utetezi, uliwakilishwa na mawakili Mohamed Salum Malik na Gabriel Malata kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Antony Kanyama na Kamaliza Kayaga waliokuwa wakimtetea Dk. Dalali Kafumu.

  Kesi hiyo ilianza kuhukumiwa jana saa 3 asubuhi na kuhitimishwa saa saba mchana.

  Akisoma hukumu hiyo, Jaji Shangali alisema Mahakama imeridhika na upande wa mlalamikaji katika malalamiko yake saba, ambayo alisema yanathibitika na kuonyesha kuwa uchaguzi huo mdogo wa Jimbo la Igunga haukuwa huru na haki.

  Alitaja baadhi ya kasoro zilizopelekea kutenguliwa kwa uchaguzi huo, kuwa ni pamoja na ahadi iliyotolewa na Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli, kwamba kama wananchi hawatamchagua mgombea wa CCM, Daraja la Mbutu ambalo ni muhimu jimboni humo, halitajengwa.

  Inasemekama Magufuli alitoa ahadi hiyo huku akijua kuwa wananchi wa Igunga wana shida zinazoweza kutatuliwa na uwepo wa daraja hilo.

  Alisema pia kwamba, Dk. Magufuli alitumia nguvu na kuwatisha wapiga kura, kwamba kama hawatamchagua mgombea wa CCM katika uchaguzi huo, watawekwa ndani, kitu ambacho Jaji alisema kilisababisha uchaguzi huo kutokuwa huru na wa haki.

  Mwingine aliyesababisha uchaguzi huo kutenguliwa ni Mbunge wa Tabora Mjini, Ismail Aden Rage (CCM), ambaye alidaiwa kutumia lugha ya uongo kwa lengo la kupotosha wapiga kura.

  Kwa mujibu wa Jaji Shangali, Rage aliwaambia wananchi wa Igunga kuwa, Mgombea wa Chadema amejitoa katika uchaguzi huo na kwamba alifanya hivyo kwa kutumia gari lake. Pia alisema kwamba, kosa hilo alilolifanya Rage kisheria angestahili kufungwa jela miaka miwili.

  Alisema pia kwamba, mbunge huyo alihusika katika vitendo vya kujenga hofu kwa wapiga kura baada ya kupanda jukwaani na bastola wakati akihutubia mkutano wa kampeni. Inasemekana kitendo cha Rage kupanda jukwaani na silaha hiyo, kiliwafanya wapiga kura kuhofia na hivyo kuleta dosari katika uchaguzi huo.

  Mbali na sababu hiyo, nyingine iliyokuwa chanzo cha kutenguliwa kwa matokeo hayo ni kitendo cha waumini wa dini ya kiislamu kuwashawishi waislam waiichague Chadema.

  Katika hoja hii Jaji huyo wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Tabora, alionyesha kusikitishwa na kitendo kilichofanywa na imamu wa Msikiti wa Ijumaa wa Igunga, Sheikh Swaleh Mohamed, kutangaza msikitini kwa waumini wa dini ya kiislamu, kuwa wasikichague CHADEMA kwa sababu viongozi wake wamehusika kumdhalilisha aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatma Kimario. Kwa sasa Kimario ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Mkoa wa Pwani.

  Sababu nyingine ni kauli iliyotolewa na Katibu Mkuu wa CCM, Wilison Mkama, kwamba CHADEMA, wameingiza makomandoo katika Wilaya ya Igunga kwa lengo la kuvuruga uchaguzi huo mdogo. Kwa mujibu wa Jaji Shangali, kauli hiyo haikuwa nzuri kwa kuwa iliwatisha wananchi.

  Pamoja na sababu hizo, nyingine ni kitendo cha Serikali kugawa mahindi ya msaada kwa wakazi wa Igunga katika kipindi cha kampeni wakati hakukuwa na mtu aliyekuwa amefariki kwa sababu ya njaa.

  Katika tukio hilo, Jaji Shangali alihoji kulikuwa na umuhimu gani wa kugawa mahindi katika kipindi cha kampeni..

  Kutokana na kasoro hizo, Jaji Shangali alitangaza rasmi kutengua matokeo ya uchaguzi mdogo wa jimbo hilo na kuiagiza Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kufuata taratibu za kufanya mchakato mwingine wa uchaguzi katika jimbo hilo.

  Aliuagiza upande wa walalamikiwa ambao ni Msimamizi wa Uchaguzi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na aliyekuwa Mbunge wa Igunga, Dk. Kafumu, kulipa gharama zote za kesi hiyo.
   
 3. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #3
  Aug 22, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hiyo imeshatoka tena, tutafute mjadala mwingine.
   
 4. PROFESA KYANDO

  PROFESA KYANDO Member

  #4
  Aug 22, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 81
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  [h=6]wetu
  [/h][​IMG]  LikeUnlike · · Share
   
 5. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #5
  Aug 22, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,843
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  Operation Sangara huko Morogoro itakuwa EPIQ MOTO kwa kichagizo cha Ushindi mahakamani.Dr.Slaa tunamuomba amualike Mwl.Kashindye awasalimia wanachi siku ya kuhitimisha kampeni pale Morgoro mjini.Ni ombi letu kwa Dr.slaaa
   
 6. K

  Kifarutz JF-Expert Member

  #6
  Aug 22, 2012
  Joined: Aug 7, 2012
  Messages: 1,695
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  One in a million
   
Loading...