CCM & CHADEMA + vyama vyote vya siasa tafakarini hili


B

brayhuss

Member
Joined
Mar 29, 2015
Messages
15
Likes
9
Points
5
B

brayhuss

Member
Joined Mar 29, 2015
15 9 5
Kwa kipindi cha siku kadhaa kumekuwa na hali ya kurushiana vijembe kutoka pande mbili za siasa yaani chama tawala na upinzani baada tu ya Lazaro Nyarandu kuhama chama.

Napenda nitoe mtizamo wangu kwa kujiuliza haya....

CCM
1. Ya nini kumsemea nyalandu ubaya baada tu ya kuondoka?
2. Kama alikuwa hafai ya nini kukaa nae bila kumfukuza?
3. Kama kuhama ni haki yake basi mpongezeni tu na aende kwa amani
4. Akiwa kwako mzuri ila akiondoka ni mbaya?
5. Acha upinzani wajipongeze maana kwao ni input na kwenu ni loss.

UPINZANI
1. Lini nyalandu alitubu makosa yake mliyomtuhumu?
2. Kwani mtu akihamia upinzani anasafishika makosa yake??
3. Nyalandu ni lini alijaribu kuhoji hadharani uongozi mbovu wa serikali?
4. Tumuiteje shujaa baada ya kukimbia ndipo aseme ubaya wa kipenzi cha mwanzo?
5. Je nyalandu hakuwepo kati ya walioipinga katiba ya warioba? Why now??

Wapendwa watanzania wenzangu tusitukanane cha msingi tuchukue hatua kutafakari pande zote kwani kila mtu ana haki yake na utashi wake.
 

Forum statistics

Threads 1,238,345
Members 475,888
Posts 29,317,480