CCM,CHADEMA na CUFU!Kuna uchafu wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM,CHADEMA na CUFU!Kuna uchafu wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Eiyer, Oct 5, 2012.

 1. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,676
  Trophy Points: 280
  Najua wakati mwingine ni vigumu kueleweka kwa watu wenye mihemko ya kihisia.Lakini wacha niseme hili ninaloamini ni sahihi.Sote tunajua namna Tanzania ilivyo leo,tuna changamoto nyingi kiasi kwamba tumekua kama mtu mwenye njaa kali ambae akipewa chochote kinachoitwa chakula,uwezekano wa kukagua usafi wa chakula kile ni mdogo sana,yeye anajali kushiba.Naam liwalo na liwe!Hapa ndipo ninapojiuliza kuhusu matumaini ya Watanzania kupelekwa kwenye Tanzania yenye neema na CCM,CHADEMA au CUF,nimechagua vyama hivi kwakuwa ndo vinavyouzika na Watanzania wengi wanavitumainia viwaletee neema.Ni ukweli usiopingika kuwa Tanzania imeharibika mikononi mwa CCM,hawana jipya na wameshindwa kabisa kuleta majibu ya matatizo yanayoikabili nchi yetu na wanaiongoza kimazoea.Sasa vimeibuka vyama hivi Chadema na Cuf,je vina majibu ya matatizo yetu?Kuna mambo yamekuwa hayasemwi kwa uwazi,hivi ni kwanini hivi vyama viwili havizungumzii ufisadi unaofanywa na viongozi wa dini?Kama kweli vinasimamia haki na usawa bila woga,ni kwanini hawagusi eneo hili?Hatuwezi kuipata Tanzania yenye neema kama hatutafuti majibu ya umaskini wetu unaposababishwa,na hapa ni moja ya eneo lililooza na linawahusu Watanzania wengi.Au wanaogopa kuwaudhi viongozi wa dini?Tunajua nguvu ya ushawishi walionayo viongozi hawa kwa waumini wao,lakini sio sababu ya kuwaogopa.Kwanini hawa hawasemwi?Kiongozi yoyote anapoanza kukwepa hoja za msingi akihofia kuudhi watu na kujipunguzia umaarufu hafai kuwa kiongozi wa kweli.Mwanasiasa anapoanza kuukwepa ukweli anakua ni adui wa ukweli.Chadema na Cuf hawasemi ukweli na ufisadi wa viongozi wa dini,wanaogopa ushawishi wa hawa watu 2015!
   
 2. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mkuu hii thread yako ina paragraph ngapi?
   
 3. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,676
  Trophy Points: 280
  Hivi ndivyo ulivyoelewa?
   
 4. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Useless thread Haina kichwa wala miguu! Leave alone paragraphs do not exist
   
Loading...