CCM Busanda inachekesha! 25-10-2010


Vincent naona akili yako imechakachuliwa. Hivi vyama vinapowagharimikia wananchi kwenda kwenye mikutano na wewe unaona ni sahihi, lazima tuushakie mfumo wako wa ubongo. kama huwezi kuona tatizo katika hilo ndiyo maana wananchi wa Tanzania wameanza kuchagua viongozi ambao ni wafadhili wa wananchi badala ya kuwaongoza.

Zamani tulifahamu wanachama katika vyama mbalimbali huvichangia vyama vyao kwa njia ya ada nk. lakini siku hizi chama ndicho kinachowachangia wanachama. Tumeona kila anayetafuata nafasi ya uongozi anatafuta fedha(mtaji) utafikiri anataka kuanzisha kampuni.

Ndugu yangu kama unafikiri ni kitu cha maana kwa chama kuwasafirisha watu ili wahudhuriea kampeni basi hali yako na kizazi chako ni mbaya. Lazima ujiulize hicho chama kinapata wapi fedha za kutumia katika matumizi ya aina hiyo? na watazirejeshaje baadaye fedha hizo kama wamekopa? Kama chama kina fedha za namna hiyo, na serikali je si zaidi? kama fedha zipo za kutosha namna hiyo kwenye mikutano ya kampeni kuna mantiki yoyote ya kuwaambia watu kwamba elimu bure haiwezekani?

tuchukue mfano mdogo: watu wamesombwa na magari kwenda kwenye kampeni na kulipwa sh.5,000. Mgombea ameweza kufanya hivyo au chama chake kimeweza kufanya hivyo kwasababu kina fedha. Mmoja wa wanaohudhuria mkutano ameshindwa kulipa ada sh.20,000 ya mtoto wake anayesoma shule ya kata. Huyo mwananchi anapofika kwenye mkutano anaambiwa kuwa elimu bure haiwezekani. Je, mwananchi huyo kama ana akili timamu ataamini hayo?
 
ccm is like an expired goods which has no value inthe market
 
Sitegemei kupata riziki yangu kupitia sanduku la kura, sheria ya gharama za uchaguzi siyo RELEVANT. Labda sheria ya makampuni na zile za kodi ndizo nahitaji kuzielewa nisibamizwe
Sasa unatafuta nini kwenye jukwaa hili? kwa nini comments zako usipeleke jukwaa lenu wafanya mizaha aka wafanya biashara? Ovyoooooooooo
 
Na bado, watabeba mpaka basi, ila kiama chaja
 


kwani wagombea huko ni nani na nani?
 
Hivi ina ruhusiwa hayo maroli makubwa kubeba binadamu (abiria) ?au kwakuwa sisiem sheria imezikwa kwa mda kwanza?
 
jana nilishuhudia mkutano wake wa ngudu...kwanza hakuwa na watu wengi na hao wachache waliokuwepo waliletwa na malori na mabasi...tena yalikuwa yamepaki pembeni yake. kingine cha ajabu kulikuwa na watu kibao wanaangalia choppers mbili ambazo zilimleta muheshimiwa, wala hawakutaka kumsikiliza.....Leo tunaye jijini mwanza kuanzia saa nane pale nyamagana
 

Tumeishawazoea. Kwanini watz bado wanakubali kubebwa katika maroli na kupelekwa ambako hawakupanga kwenda?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…