CCM bado ni chama cha kijamaa?

CCM bado ni chama cha kijamaa?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,162
Reaction score
48,429
Niliangalia ile harambee yao na jinsi wanavyoendesha chama chao, nikajiuliza kama CCM bado kina sifa ya kuendelea kuitwa chama Cha kijamaa...

CCM bado ni chama cha wakulima na wafanyakazi ama ndiyo kimeshakuwa chama cha MABEPARI na wafanyabiashra?

Ubeberu umetamalaki CCM😄😆😀
 
Yes,
ni chama cha kijamaa tena ni ule ujamaa wa kisasa kabisa, wenye umoja zaidi, udungu zaidi, uwazi zaidi, usawa zaidi na usie thubutu kumuacha binadamu hata moja nje ya familia hii pana na madhubuti sana ya CCM kijamii, kisiasa na hata kiuchumi.

Kazi na utu, tusonge mbele pamoja bila chuki bali umoja na mshikamano wa kitaifa na kimataifa.
Hiyo ndio CCM gentleman chini ya Dr.Samia Suluhu Hassan 🐒
 
Miaka 5 iliyopita, mgimbea wao- JPM alikataa michango ya matajili kama Mzee Mengi, ajabu leo hii ndio wanao alikwa kuja kuchangia bil 100 na msajili anawapa baraka kwamba wazitumie kama itavuyo wafaa... miaka 5 ijayo baada ya 29/10/2025, nchi hii itakuwa mshike mshike kwa sana..
 
Marajiri ndio waajiri na walipa kodi wakubwa

Mtu kukataa michango yao anakuwa kichwani hazimo

Kuwa tajiri sio kosa
 
CCM halisi ya wazazi na mababu zetu asili yake ni ujamaa isipokuwa wanaokiendesha sasa na kukisimamia ni mabebari waliojificha katika ujamaa kwa lengo la unyonyaji na ukandamizaji wa wananchi wasiojitambua.
 
Niliangalia ile harambee yao na jinsi wanavyoendesha chama chao, nikajiuliza kama CCM bado kina sifa ya kuendelea kuitwa chama Cha kijamaa...

CCM bado ni chama cha wakulima na wafanyakazi ama ndiyo kimeshakuwa chama cha MABEPARI na wafanyabiashra?

Ubeberu umetamalaki CCM😄😆😀
Siyo tu cha kijamaa; ni chama cha watu weusi? Au cha Waasia? CCM ni katawi tu ka Jamaat el Hindu, full stop
 
Marajiri ndio waajiri na walipa kodi wakubwa

Mtu kukataa michango yao anakuwa kichwani hazimo

Kuwa tajiri sio kosa
Hapa tunazungumzia itikadi, falsafa na sera za CCM. Wajamaa na mabepari wote huajiri... Tofauti yao ni hizo sera zinazotokana na itikadi inayoundwa na falsafa ya chama.

Matajiri huo utajiri wameupataje kwenye nchi ya kijamaa?
 
Imani Na. 3 ya CCM, inasema chama kinaamini kwamba:
Ujamaa na kujitegemea ndiyo njia pekee ya kujenga jamii ya watu walio sawa na huru.
 
Unajua maana ya chama cha kijamaa? Au unatafsiri kama wale wahuni kuhusu ujamaa?
Ni rahisi mno kuielewa na kuzitafsiri familia hii madhubuti sana ya CCM ambayo haibagui mTanzania yeyote kwa rangi yake, kabila lake au dini yake. Haimdharau mwanadamu yeyote wala kumuheshimu mtu eti kwasababu tu ya utajiri au umaskini wake, bali inajali thamani ya utu wa kila mwanadamu regardless ya mirengo yao ya kisiasa.
Hiyo ndio CCM ya kisasa ya kijamaa.

CCM ni muunganiko wa familia zote za waTanzania ndio maana haiyumbi wala kuyumbishwa na vibaraka, vibaka au matapeli wa kisiasa wanamfadhiliwa na mabwenyenye ya magharibi 🐒
 
Ni rahisi mno kuielewa na kuzitafsiri familia hii madhubuti sana ya CCM ambayo haibagui mTanzania yeyote kwa rangi yake...
Vyama vya siasa hubagua watu kutokana na misingi ya itikadi zake. Huwezi sema Democratic ya Marekani inafafana kisera na Republican.

Wakati republican hupendelea Serikali ndogo ya shirikisho (Federal Government) Democratic wao ni kinyume chake.

Sasa kama hakuna ubaguzi wa kisera ni kwa nini tuna vyama vingi tofauti?
 
wanaofadhiliwa na mabwenyenye ya magharibi 🐒
Kwa ivo kufadhiliwa na mabwanyenye wa ndani ni salama zaidi kuliko hao mabwanyenye wa magharibi?

Hao mabwanyenye wa ndani hawana uhusiano na hao mabwanyenye wa magharibi?

Ukishaanza kukumbatia mabwanyenye iwe wa ndani ama wa nje, uhalali wa kuwa chama cha kijamaa unapotea
 
ndio maana baadhi ya waropokaji wanaofadhiliwa na mabwenyenye ya magharibi hivi sasa wanasota korokoroni kwasababu walipoteza uelekeo right?🐒
 
Vyama vya siasa hubagua watu kutokana na misingi ya itikadi zake. Huwezi sema Democratic ya Marekani inafafana kisera na Republican.

Wakati republican hupendelea Serikali ndogo ya shirikisho (Federal Government) Democratic wao ni kinyume chake.

Sasa kama hakuna ubaguzi wa kisera ni kwa nini tuna vyama vingi tofauti?
Chadema mathalani ilibagua mno watu ambao sio wachaga lakini pia haikupendelea wanachama wasio wakristu.

hata chadema masalia ya sasa,
inapendelea zaidi watu wa singida na bado kuna kasumba ya kubagua wasio wakristu inaendelea.

ndio maana unamuona father Kitima wa kanisa katoliki anavyojaribu kuingiza chadema ndani ya kanisa katoliki kwasabb tu Lisu ni msingida wa kabila lake n.k.

huwezi kukuta mambo ya hovyo kama hayo ndani ya familia ya kijamaa ya CCM, ndio maana inafahamika kwamba CCM ni ya waTanzania wote 🐒
 
Back
Top Bottom