CCM badilisheni mbinu, kwa hii mnajiaibisha!

Namichiga

JF-Expert Member
Jun 1, 2017
356
524
Ndugu zangu hakuna jambo gumu kama mabadiliko kwa maana ni jambo ambalo haliji kiwepesi kama kukoroga sukari kwenye chai.

Wakati mh. Rais Magufuli anakabidhiwa madaraka, kichwani kwake alishajichorea twasira ya Tanzania anayoitaka.
Jambo hili si baya lakini alichokosea ni kudhani kwamba marais wote waliopita ni wazembe na hawakuujua wajibu wao, hali iliyopelekea kuingia ofisini huku imemjaa dhihaka,kebehi na majigambo yaliyopitiliza.

Lakini cha ajabu miaka mitano ya kwanza inayoyoma lakini hali ya mwananchi wa kawaida yamezidi kudidimia.Japokua yapo yaliyofanyika lakini kiuhalisia hayajagusa maisha ya watu kule mtaani.

Kitengo mahususi cha propaganda muda mwingi kiko kazini kuimba nyimbo za kusifu ambazo mwananchi wa kawaida anashindwa kuzielewa!
Wanataja ndege, reli, bwawa la umeme, vyeti feki na mengineyo. Lakini mwananchi wa kule Namtumbo, Mangaka, Tandahimba, Newala, Nachingwaea Liwale, Manyoni, Bariadi na kwingine kwingi maisha bado ni magumu sana.
Ananunua unga, sukari na mahitaji mengine kwa bei ya juu na kipato ni kigumu sana.

Hivyo mwananchi huyu jukwaa lake alillokua analingoja kwa hamu ili kufikisha hisia na maoni yake ni uchaguzi tu!, kwani hapa ndipo wanapoweza kumjibu mzee kwamba mnachokilazimisha kiimbwe sicho hivyo tunawakataa watu wako kwenye sanduku!.

Hali hiyo chama changu CCM walishaijua kwani alam ilishagonga, hapo ndipo walipoamua kuja na mbinu ya kupita bila kupingwa ili kuvuna ushindi wa kishindo na hatimaye kuutangazia ulimwengu kwamba Mh. Rais anakubalika!

Lakini matokeo yamekua ndivyo sivyo, kwani licha ya plan yao kufanikiwa lakini mkakati wa utekelezaji ulikua dhaifu hivyo umezua viroja vya zahiri.

Hivyo nakiomba chama changu kibadili mbinu kwani kwa mbinu hii kinajidhalilisha na kujishushia heshima ya kuwa chama kikongwe na chenye wigo mpana wa mbinu za kushika dola.
 
Sana chama dharimu kisichojiamini kinachotumia mabavu kubaki madarakani..
Na hii itapelekea kutengwa kimataifa kama Zimbabwe .
Tawala za mabavu zilishapita zamani zimebaki chache sana.
 
Jiwe amezaliwa na amekulia kwenye dhuluma, kamwe hawezi kukuelewa kuhusu suala la kukandamiza demokrasia.

2015 tuliingia chaka sana kumkabidhi nchi mtu mwenye roho ya jiwe. Na nina wasi wasi sana kama hata akimaliza miaka kumi atakubali kuondoka. Maana ameiteka nchi, serikali, chama na sasa anapoka hata haki ya kuchagua toka kwa wananchi.
 
Kumbukeni mabavu ni dalili ya kukosa ushawishi au kilushindw..
Niwape mfano relevant.. Mbakaji anaamua kubaka kutokana na kukosa ushawishi kwa yule mengwa so anaona no way but to force !
 
Tuna mbinu zaidi ya 1000 ndio kwanza tumetumia 00000.1

State agent
Yaani we unajiita 'state agent' alafu unakubaliana kweli na huu upuuzi uliofanyika kwamba nayo ni miongoni mwa hizo mbinu 1000. Basi mtakuwa mmeishiwa mbinu, acheni kutumia vilaza kuwapangia mbinu zenu.

Wenzenu hutumia vipanga ambao wakipanga mpango hujiuliza na maswali ya mbele na kuyatafutia majibu yake. Wakiona mpango hauna majibu mazuri wanaachana nao wanatafuta mwingine. Sio nyie eti waalifu wamekimbia wameacha bunduki wameshindwa kuchoma gari moto. Au kama hivi sasa mnavyo haha kuwalazimisha ACT na CHADEMA kushiriki uchaguzi kwa lazima mnaona aibu mbinu zenu zimekuwa mbovu zinastukiwa hata na kichaa.
 
Back
Top Bottom