CCM Arusha wamjibu Lowassa sakata la msiba wa wanafunzi Lucky Vincent

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,999
CCM Arusha wamjibu Lowassa sakata la msiba wa wanafunzi Lucky Vicent

Chama cha Mapinduzi mkoa wa Arusha kimeishangaa kauli ya aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa kusema kuwa Rais John Magufuli amemtuma ‘mtoto mdogo’ kwenda kuiwakilisha serikali kwenye mazishi ya wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Michael Lekule ,amesema kauli ya Waziri huyo mstaafu ameitoa kwa kudanganya wananchi na kuonesha serikali ya Magufuli haishirikiani na wananchi ,wakati serikali iliubeba msiba huo mzito wa taifa.

Amesema jitihada za serikali ya Magufuli zimeonekana kupitia kwa wawakilishi wake Makamu wa Rais Samia Suluhu pamoja na Mrisho Gambo pamoja na wanachama wa CCM ambao walijitokeza kwa wingi kwenye msiba huo mzito

"Serikali ilijitoa kwa hali na mali kuwezesha familia 35 kwenda kupumzisha wapendwa wao,na ilihakikisha kila mwili unapumzika mahala popote familia inapopata,tunajiuliza walitaka nini kama kote nafasi ilijazwa na serikali ya Magufuli," alisema Michael

"CCM inakanusha kwanguvu upotoshaji huo,hata ukiangalia siku ile uwanja wa shekh Amri Abeid wanaccm walijaa uwanjani ,kikubwa CCM imeguswa na msiba uliotokea na Rais wetu amekuwa bega kwa bega juu ya tukio lililotokea,"amesema

Pia amesema wamemshangaa kwa kusema Rais alimtuma mtoto mdogo wakati yeye mwaka 2007 ajali mbaya iliyotokea Monduli duka bovu na kuua watu 20 ambao 11 walikuwa ni askari wa JKT,rais Kikwete alimtuma aje kuiwakilisha serikali.

Hata hivyo alimtaka kiongozi huyo, ajiulize kama yeye kipindi akiwa Waziri Mkuu aliweza kutumwa na Rais, amuwakilishe kwenye msiba wa watu 20, je yeye na Makamu wa Rais ni nani mdogo?

"Tena ajali hiyo ilikuwa ya kitaifa,askari 11 walifariki kwenye ajali,mbona hajayasema ya kwake?," amesema Lekule

Chanzo: Mwananchi
 
Soma Zaidi:http://www.mwananchi.co.tz/…/1597578-3932416-ld7…/index.html

How much are you paid for this laborious task of posting after every 1 minute!
 
CCM Arusha wamjibu Lowassa sakata la msiba wa wanafunzi Lucky Vicent

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Michael Lekule ,amesema kauli ya Waziri huyo mstaafu ameitoa kwa kudanganya wananchi na kuonesha serikali ya Magufuli haishirikiani na wananchi ,wakati serikali iliubeba msiba huo mzito wa taifa.
Soma Zaidi:http://www.mwananchi.co.tz/…/1597578-3932416-ld7…/index.html

Usidanganye Umma Serikali haijafanya chochote maana gharama zote zimebebwa na Michango.

Kawaambie Watanzania hatudanganyiki kizembe hivyo.
 
Huyu babu Lowassa angestaafu tu haya mambo ya siasa....
kiufupi unataka anyamaze..siasa ni maisha...na maisha yake yote amekuwa mwanasiasa.

bro...nakushauri na wewe ustaafu kuongelea siasa maana tangu msukuma mwenzako aingie ikulu umekuwa kitu cha ajabu sana
 
CCM Arusha wamjibu Lowassa sakata la msiba wa wanafunzi Lucky Vicent

Chama cha Mapinduzi mkoa wa Arusha kimeishangaa kauli ya aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa kusema kuwa Rais John Magufuli amemtuma ‘mtoto mdogo’ kwenda kuiwakilisha serikali kwenye mazishi ya wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Michael Lekule ,amesema kauli ya Waziri huyo mstaafu ameitoa kwa kudanganya wananchi na kuonesha serikali ya Magufuli haishirikiani na wananchi ,wakati serikali iliubeba msiba huo mzito wa taifa.

Amesema jitihada za serikali ya Magufuli zimeonekana kupitia kwa wawakilishi wake Makamu wa Rais Samia Suluhu pamoja na Mrisho Gambo pamoja na wanachama wa CCM ambao walijitokeza kwa wingi kwenye msiba huo mzito

"Serikali ilijitoa kwa hali na mali kuwezesha familia 35 kwenda kupumzisha wapendwa wao,na ilihakikisha kila mwili unapumzika mahala popote familia inapopata,tunajiuliza walitaka nini kama kote nafasi ilijazwa na serikali ya Magufuli," alisema Michael

"CCM inakanusha kwanguvu upotoshaji huo,hata ukiangalia siku ile uwanja wa shekh Amri Abeid wanaccm walijaa uwanjani ,kikubwa CCM imeguswa na msiba uliotokea na Rais wetu amekuwa bega kwa bega juu ya tukio lililotokea,"amesema

Pia amesema wamemshangaa kwa kusema Rais alimtuma mtoto mdogo wakati yeye mwaka 2007 ajali mbaya iliyotokea Monduli duka bovu na kuua watu 20 ambao 11 walikuwa ni askari wa JKT,rais Kikwete alimtuma aje kuiwakilisha serikali.

Hata hivyo alimtaka kiongozi huyo, ajiulize kama yeye kipindi akiwa Waziri Mkuu aliweza kutumwa na Rais, amuwakilishe kwenye msiba wa watu 20, je yeye na Makamu wa Rais ni nani mdogo?

"Tena ajali hiyo ilikuwa ya kitaifa,askari 11 walifariki kwenye ajali,mbona hajayasema ya kwake?," amesema Lekule

Chanzo: Mwananchi
Majibu Mujarabu.

Mkuu wa Manyumbu kaumbuka
 
Back
Top Bottom