CCM Arusha: Lema amelipotosha bunge kuhusu Arusha

CCM Arusha: Lema amelipotosha bunge kuhusu Arusha

CCM Arusha Leo wahitimisha ziara ya kutembelea kata zote za Arusha Mjini kukagua ilani ya uchaguzi ambapo pia wamefanya mikutano ya hadhara

Mikutano hiyo iliyoongozwa na MWENYEKITI Wa CCM wilaya DK SOILELI imekuwa namwitikio mkubwa haswa baada ya kupokea wanachama wengi Wa CHADEMA Kama Kata ya UNGA LTD MWENYEKITI na katibu Wa CHADEMA na kurudi CCM

Leo katika kata ya Ngarenaro mwenyekiti Wa vijana Wa CCM wilaya ya Arusha Mjini amemwinya LEMA kuacha kuwaongopea wajumbe Wa bunge LA katiba kuwa msimamo Wa wana Arusha ni serikali mbili na siyo tatu tatu ni za kwake yeye siyo za wanaarusha

Yeyote atakaye dhubutu kuichezea amani yetu watanzania Uvccm tutamshughulikia kikamilifu

Alimalizia kwa kuwaomba wana Arusha kuikataa CHADEMA maana wameharibu Mjini na kuwafanya watalii wasije Arusha uchumi kuporomoka kisa maandamano na mabomu ya CHADEMA

Mkataeni lema na chadema yake alimalizia mwenyekit huyo

dah umelo.g.w.a kajipange upya
kwanz hata picha ujaweka
of coz we umetuvamie
 
Wana ARUSHA tumeshaikataa CHADEMA na mambo yake yote! Huyu LEMA tunasubiria uchaguzi tu ili tumrudishe kwao Machame.

Labda itasaidia. Lakini bado najiuliza, hivi kama pamoja na kutumia ofisi za Mkuu wa Mkoa na DC vibaya, pamoja na kutumia Polisi katika kulazimisha ushindi Arusha, kama pamoja na kuua watu kwa risasi na mabomu, na kama pamoja na kuwafunga na kuwasingizia kesi kila siku, Arusha uchaguzi ndiyo ulikuwa vile tulivyoona, itakuwaje pale mtakapokuwa wenyewe, bila polisi wala yeyote nyuma yenu?

Nna uhakika kama siyo polisi, jeshi na usalama CCM ingeshatolewa madarakani. hivyo hata huko mlikoshinda mnapaswa kuona aibu kwani ndani ya nafsi zenu mnajua wananchi wamewachoka na hawawapendi.
 
Lema ni mropokaji tu hana lolote, ipo siku wanaarusha wataligundua hili.

Ila we unaonaje? Mi naona ni heri mropokaji mwenye ridhaa ya wananchi kuliko, watu waliopiga wananchi mabomu na risasi kulazimisha kuchaguliwa, na bado pamoja na damu kumwagika bado wakamchagua mropokaji huyo! Huenda ni dalili kuwa anachokiropoka kiko katika lugha wanayoielewa wana Arusha. Nadhani pia ni muda wa wanaCCM kuanza kufikiria na hili. That is called thinking big.
 
Ahsante kwa kukubali kua ni mropokaji, ipo siku atatokea hu walks the talk ndo itakua mwisho wa huyo jamaa
 
Labda itasaidia. Lakini bado najiuliza, hivi kama pamoja na kutumia ofisi za Mkuu wa Mkoa na DC vibaya, pamoja na kutumia Polisi katika kulazimisha ushindi Arusha, kama pamoja na kuua watu kwa risasi na mabomu, na kama pamoja na kuwafunga na kuwasingizia kesi kila siku, Arusha uchaguzi ndiyo ulikuwa vile tulivyoona, itakuwaje pale mtakapokuwa wenyewe, bila polisi wala yeyote nyuma yenu?

Nna uhakika kama siyo polisi, jeshi na usalama CCM ingeshatolewa madarakani. hivyo hata huko mlikoshinda mnapaswa kuona aibu kwani ndani ya nafsi zenu mnajua wananchi wamewachoka na hawawapendi.

Mkuu, Acha kujidanganya kuwa CCM imechokwa! Uchaguzi wa mwaka 2010 CHADEMA iliambulia majimbo 23 kati ya majimbo yote ya uchaguzi Tanzania. Uchaguzi wa marudio wa Udiwani kata 27, CHADEMA ilipata kata 3 tu! Kalenga na Chalinze unajua kilichotokea. Kusema CCM imechokwa ni kujitoa ufahamu tu!
 
Na huyo Soileli ni nani kamwambia Arusha wanataka Serikali 2?

Maoni ya wananchi ni Serikali 3,so Lema anatuwakilisha vyema.

Ziara ya kutembelea kata zipi? Mbona Kimandolu na Baraa hatujawaona?

Hiyo ziara itakuwa iliishia ktk Mirungi mtaa wa Makaburi ya Baniani Unga ltd kwa diwani wa Magamba Issa.

kula like yangu mkuu,haya majitu maongo sana
 
Mkuu, Acha kujidanganya kuwa CCM imechokwa! Uchaguzi wa mwaka 2010 CHADEMA iliambulia majimbo 23 kati ya majimbo yote ya uchaguzi Tanzania. Uchaguzi wa marudio wa Udiwani kata 27, CHADEMA ilipata kata 3 tu! Kalenga na Chalinze unajua kilichotokea. Kusema CCM imechokwa ni kujitoa ufahamu tu!

Sure! Imagine the type of victory when police, TISS and Green guard criminals were a part of your winning teams! how dare you call that a victory? If you were men enough why didn't you go out there by yourselves to win?

I think that has jogged your memories a little. Now start thinking afresh, and come back with right answers!

Unaongelea majimbo mliyoshinda? Na ilikuwaje wizi wote wa kura uliotokea uchaguzi huo uliilenga CCM? Ile ni dalili tosha kuwa CCM imechokwa. Huo ndiyo ukweli. Vinginevyo kama mnapendwa kama unavyotaka kuita, nendeni kwenye kampeni kama CCM, msiihusishe polisi wala jeshi. Na muwaache Usalama. Halafu muache kuasisi vurugu na kumwagia watu tindikali huku mkiwasingizia upinzani, Muache kung'oa watu kucha na meno. Halafu muone kama mtashinda majimbo mangapi! Vinginevyo wanaume wanaojiamini huwa hawaibi kura, wala kulazimisha matokeo kwa kutumia vyombo vya dola!

By the way CHADEMA kupata kata 3 ambazo zilikuwa za CCM huku ikitetea kata zake zote huo ni ushindi mkubwa, in case unajua hesabu za kujumlisha na kutoa. Na kwa maoni yangu, Kwa matokeo ya chaguzi zote na tabia ya CCM na serikali yake kuudidimiza upinzani, ni sawa kabisa kusema CHADEMA pamoja na wapinzani walioshinda ni wanaume wa shoka. Kwani pamoja na Tume ya uchaguzi ya CCM, polisi, jeshi na usalama wa CCM, bado kuna vidume vimeshinda majimbo na kata kadhaa! Wewe unaonaje hiyo? Ningekuwa mimi hata nisingeongea.
 
Kwa hiyo, kwa kutumia akili ndogo tu, nani hapo ndiyo wa maana na mkweli? Ni Godblee Lema ambaye amechaguliwa kwa kura za kutosha kuwa mbunge wa Arusha Mjini au Mwenyekiti wa vijana wa chama kilichoshindwa uchaguzi? Au mnaonaje kwamba hata hao wananchi walioichagua CHADEMA na kuipa viti karibu vyote vya udiwani siyo sehemu ya Arusha? Au UVCCM Arusha nayo ina mamlaka ya kuwasemea na hao, tofauti na kura zinavyosema?

Ni kweli kuwa CCM ni mpaka uwe na kasoro kichwani! Hivi kati ya CCM na CHADEMA nani ndiyo chanzo cha mabomu ya Arusha? Kama siyo upuuzi wa serikali ya CCM kulazimisha ushindi na kunyanyasa upinzani nani angekufa Arusha? Acheni kulazimisha maoni hata pale mnapojua wananchi wana maoni tofauti. Lema kwa sasa ni sauti ya Wana Arusha. Mpaka atakapopewa ubunge mtu mwingine, ni busara mkamheshimu na kushirikiana naye kufanya maendeleo ya Arusha.

Nadhani pia kunatakiwa kuwe na muda wa kampeni na muda wa kujenga nchi. Kwa ninavyokumbuka, muda wa kampeni umepita. Hebu waacheni wana Arusha wajenge Arusha yao.

milipuko yote inayotokea arusha ni project za ccm!
 
Ahsante kwa kukubali kua ni mropokaji, ipo siku atatokea hu walks the talk ndo itakua mwisho wa huyo jamaa

Siyo mropokaji, ongezea "mwenye ridhaa ya wananchi" Because that right there, is the difference between loosing and winning! By the way angekuwa mropokaji sidhani kama angechaguliwa. Una maana wewe tu ndiyo umeona ni mropkaji halafu wote waliompigia kura hawajaona hilo? Au wana Arusha wote ni wajinga ila wewe tu ndiyo umewazidi akili? Na inawapa shida gani kama wana Arusha wameona inafaa kuongozwa na "mropokaji" kama unavyotaka watu wakuelewe? Na kwa unavyoonekana ni wazi unawajua watu kadhaa ambao siyo waropokaji akiwemo yule mama aliyegombea nafasi ya ubunge. Ilikuwaje hao wasio waropokaji wakashindwa? Au milidhani kuwa na mabodyguard wa kijeshi ndiyo dili?

By the way sijawahi kuona serikali inatumia nguvu nyingi kwa kumtumia polisi, kupiga mabomu wananchi mikutanoni na kulazimisha Usalama wa CCM wasilale, kisa mropokaji flani! Halafu mbaya zaidi, pamoja na kumwaga damu, na kutumia nguvu zote, bado mnazidiwa! Unadhani bila kutumia vyombo vya dola mngekuwa na hali gani? Hilo jibu baki nalo kwani wote tunajua litakuwa jibu gani.
 
Back
Top Bottom