CCM adui yenu si CHADEMA bali ni.......

babalao 2

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
5,392
3,201
Mjadala mkubwa hapa nchini ni juu ya vyama viwili CCM na CHADEMA.
CCM kwa nguvu zote wanajitahidi kutuaminisha kuwa adui yao ni adui wa Watanzania wote ambae ni CHDEMA. Wao wanadai CHADEMA husema kwamba CCM hawajafanya kitu cha maana ktk ujenzi wa Taifa bora la Tzania zaidi ya kufisadi rasilimali za taifa. Hii huonekana katika vikao vya ndani na majukwaani lazima utasikia wakisema CHADEMA lengo lao ni kuvuruga amani na pia wanarudisha nyuma maendeleo ya nchi hivyo wasipate nafasi ya kuongoza nchi.

Kwa upande wa CHADEMA wao husema wazi ya kuwa adui namba moja kwa watanzania ni CCM japokuwa tuliaminishwa na BABA WA TAIFA KUWA MAADUI WETU NI MARADHI UJINGA NA NJAA wao husema yote hayo husababishwa na UFISADI. Ufisadi huo umesimikwa na CCM na umekuwa sugu mpaka wao CCM wameufananisha na GAMBA. Falisafa ya CHADEMA wanasema ukiuchukia ufisadi ni sawa na umeichukia CCM na ukichukua CCM ni sawa na kuchukia ufisadi. Matatizo ya nchi hii ni MATOKEO YA URAFIKI WA CCM NA UFISADI.

MFANO kuna watu ndani ya CCM waligundua kuwa adui wa CCM ni UFISADI na wala si CHADEMA hakika walipata maonyo makali na kuombwa wahamie CHADEMA ili wasemee Ufisadi wakiwa nje.

CCM ADUI YENU SI CHADEMA NI UFISADI MLIOUKUMBATIA.
 
Olaigwanani lang

JF-Expert Member
Apr 26, 2012
520
139
Kukithiri kwa rushwa nchini kukiongozwa na chama tawala ccm...............CHADEMA INAHUSIKA.Uteuzi usiofaa wa mawaziri na watendaji wakuu wa serikali...................... CHADEMA INAHUSIKA.Serikali kutokuwa na nia ya kuendeleza nchi.......................... ......CHADEMA INAHUSIKA.kuendeleza mfumo dhaifu wa uchaguzi na uchakachuaji kura.......... CHADEMA INAHUSIKA.Kuongezeka kwa ukosefu wa ajira......................... ........................CHADEM A INAHUSIKA.Kushuka kwa kiwango cha elimu nchini........................ ..................CHADEMA INAHUSIKAMatukio ya kuzama kwa meli na ajali za Barabarani....................................................................................CHADEMA INAHUSIKA.Na kadhalika nakadhalika........nakadhalika .............................. ..... CHADEMA INAHUSIKA.Jamani, ccm na serikali yake, jifunzeni kuwa wa kweli na kukubali udhaifu wenu. Katika hila na uwongo hakuna nia njema.
 
Mr Rocky

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
15,181
14,319
Swali moja tuu jepesi kwa viongozi ambao wanatumia nguvu nyingi sana kutetea kuwa huyu ana kadi ya CCM mara anailipia mara hajawahi kuondoka kwenye hicho chama ina manufaa gani kwa mwananchi ambaye anaishi kwa mlo mmoja kwa siku
Inasaidia nini9 kuondoa ufisadi ambao umepatakaa hapa nchini karibu kila kona
Inasaidia nini kwa mmwananchi ambaye korosho zake analipwa bei chini ya kiwango na hapati hata mnunuzi na mnunuzi ambaye ni mlanguzi akimfikia anamkopa
Inasaidia nini kwa mfumuko wa bei uliopo kwa sasa ambao ni wa kutisha
Inasaidia nini kwa mgao wa kisirisiri wa umeme tulio nao
badala ya kupambana ili maisha ya wananchi yafanikiwe na serikali isimamiwe katika utendaji wake wa kazi watu wanabishana kuhusu kuwa na kadi za chama
Kuhusu CDM na harakati zake
Je kama chama tawala mnafanya nini kuboresha maisha ya wananchi na sekretarieti yenu mpya imekuja na mikakati gani au bado mnapambana na CDM na kumuona ndie adui wa watanzania kutokuwa na maisha bora ni adui wa watanzania kwa kuleta mfumumo wa bei na kuendeleza ufisadi na wizi wa rasilimali za taifa na CDM ndo wanaowalea mafisadi wa nchi hii
 
  • Thanks
Reactions: dkn

Na hawa waandishi wanaouwawa na polisi na kujeruhiwa CHADEMA inahusika?
 
Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,980
9,547
Swali moja tuu jepesi kwa viongozi ambao wanatumia nguvu nyingi sana kutetea kuwa huyu ana kadi ya CCM mara anailipia mara hajawahi kuondoka kwenye hicho chama ina manufaa gani kwa mwananchi ambaye anaishi kwa mlo mmoja kwa siku
Inasaidia nini9 kuondoa ufisadi ambao umepatakaa hapa nchini karibu kila kona
Inasaidia nini kwa mmwananchi ambaye korosho zake analipwa bei chini ya kiwango na hapati hata mnunuzi na mnunuzi ambaye ni mlanguzi akimfikia anamkopa
Inasaidia nini kwa mfumuko wa bei uliopo kwa sasa ambao ni wa kutisha
Inasaidia nini kwa mgao wa kisirisiri wa umeme tulio nao
badala ya kupambana ili maisha ya wananchi yafanikiwe na serikali isimamiwe katika utendaji wake wa kazi watu wanabishana kuhusu kuwa na kadi za chama
Kuhusu CDM na harakati zake
Je kama chama tawala mnafanya nini kuboresha maisha ya wananchi na sekretarieti yenu mpya imekuja na mikakati gani au bado mnapambana na CDM na kumuona ndie adui wa watanzania kutokuwa na maisha bora ni adui wa watanzania kwa kuleta mfumumo wa bei na kuendeleza ufisadi na wizi wa rasilimali za taifa na CDM ndo wanaowalea mafisadi wa nchi hii

Kwa kuwa watanzania hatuko tayari kuchagua na kuchaguliwa kwa dhamira njema, kwa kuwa watanzania bado hawajajiandaa kuwachagua viongozi wenye dhamira njema na watanzania, viongozi ambao wapo tayari kuwakomboa watanzania, wenye moyo wa kujitolea kwa nguvu zote kuhakikisha maisha ya watanzania yanabadilika kuelekea kwenye neema, CHADEMA wataendelea kuwa Adui Mkubwa kwa serikali iliyopo madarakani ya ccm.
Wakati wa mwalimu kulikuwa na maadui watatu, ambao walikuwa Umaskini, Ujinga na Maradhi, lakini sasa hali imegeuka, ambapo Umaskini na Ujinga ndiyo mtaji wa serikali ya ccm, na CHADEMA anabaki kuwa Adui namba moja, angalieni mauaji ya Arusha, Morogoro, Iringa na kwingineko, yote ni kumtokomeza adui mkubwa CHADEMA.
 
Mr Rocky

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
15,181
14,319
Mungi adui wanayemuangalia sasa ni CDM ndio mwarobaini wa matatizo yao na wakifanikiwa kuiangamiza watakuwa wametatua nusu ya matatuizo ya watanzania . Hilo ndo wanalowaza na ndio kupaumbele chao kwa sasa
hawawazio kuhusu wezi wa mali ya umma wala wezi wa rasilimali zetu ila wanawaza CDM ndio kikwazo cha wao kuendelea kufanya ufisadi wao
Wanawaza namna ya kukiminya kisiwepo au watafute kashfa ambayo wataiunda ili kionekane machoni mwa watu kuwa sio chama cha maana ili waendelee kula faida na mtaji wa watanzania
Badala ya kukaa na kulpambana na wizi na ufisadi wamekaa kupambana na CDM na wanakaaa wanaongea masuala ya sijui kuwa na kadi au kutokuwa na kadi
Je mkisnamaliza suala la kadi mtarudi kwa watanzania kuwaambia kitu gani au ndo kazi ta sekretarieti mpya ya chama kuwatafuta wanachama wenu waliopotea na ambao wako kambi ya upinzani na kuwarudisha kwenu na baada ya hao naamini maisha ya Mtanzania yatakuwa yameboreka kwa asilimia mia
 
Last edited by a moderator:

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

3 Reactions
Reply
Top Bottom