Msittu
Member
- Apr 6, 2012
- 7
- 36
Kwa mizania yoyote ile, msingi wa kipimo cha mitazamo kwamba adui namba moja wa Tanzania kwa sasa ni CCM kitasalia kuwa ni falsafa ya chama hicho kikongwe.
Ukiacha falsafa yake, umri na uchama tawala ni nadharia nyingine muhimu ya ustawi wa uadui. Kushindwa kuiishi falsafa kumeunda falsafa mbadala kwa gharama ya Umma na sio wanachama wake. Gharama hizo ndio chanzo cha uadui.
Umri umebeba mambo mengi ndani yake ila kubwa ni uzazi na vizazi. CCM kwa kipindi chake imefanikiwa kuwa na uzao na kujenga vizazi ambavyo kwa namna moja ama nyingine vimezaliwa na hulka na utashi binafsi. Sifa hizo mbili zimekifanya kizazi hiki kuwa na hisia tofauti na wazazi wake pamoja na Ndugu. Huo ni msingi mwingine wa uadui.
Uchama tawala ni sehemu nyingine muhimu ya uadui. Kwa hisani ya demokrasia hili limewezekana. Utawala wa ilani, mali, watu, mitazamo na hisia zao ni msingi mkuu wa uadui.
Mwisho ni utaasisi. Hili huwenda matokeo yake yakawa bayana siku za usoni, mwenendo wa chama kukosa mamlaka ya kitaasisi umekifanya kisiwe na undugu na taasisi nyingine za kisiasa kwa ustawi wa siasa. Mtengano huo ndio unaotanua mitazamo ya uadui, matumizi ya dola ndani ya taasisi ya kisiasa ni utawala sio uongozi tena. Matokeo ya utawala huonekana bayana kwa watawaliwa kama ilivyo kwa uongozi yanavyo onekana kwa wanao ongozwa.
Ni mtazamo wa uadui utakao jenga urafiki. Adui ni rafiki wa kudumu.