Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,353
- 26,194
Kwanza mlianza na Azimio la Kujivua Gamba. Mkawataja na wanachama wenu watatu mliowapachika jina la Mapacha Watatu ambao ndio hasa walikuwa walengwa wa kuvuliwa gamba. Hao ni Edward Ngoyai Lowassa,Rostam Aziz na Andrew John Chenge. Mkawapa na miezi mitatu hao wahusika wajitoe wenyewe chamani au mtawashughulikia.
Miezi ikapita,watu wakabaki.Rostam alijivua nyadhifa zake zote ndani ya chama.Wakabaki wawili: Lowassa na Chenge. Hawa wameendelea kuwepo na kujiimarisha kiuongozi ndani ya chama na Bunge.
Sasa,katika kutoa maoni ya Katiba mpya,Lowassa na Chenge wameendeleza mchezo wao wa kuzinyanyasa akili za watanzania. Lowassa,bila kuzingatia uwepo wake Serikalini muda mrefu na uelewewa wake wa Katiba,Sheria na Kanuni,akasema kuwa eti Katiba iseme rushwa katika uchaguzi ni nini.Akamaanisha kuwa hajui 'definition' ya rushwa ya uchaguzi na wala hajawahi kuiona wala kuisikia ndani ya Katiba,Sheria na Kanuni za nchi hii. Akapigiwa makofi!
Ndugu Chenge naye,akitoa maoni ya Katiba,ameomba Katiba mpya iwadhibiti wala rushwa. Anamaanisha ya sasa haiwadhibiti na wala haiwajui. Naishiwa maneno. Kila mtu najifanya hausiki.
CCM,sisi ni watu wazima tena werevu. Tunajua angalau kusikiliza na kuelewa ingawa si waamuzi. Msitudanganye sana.Tunahitaji na ukweli kidogo. Tusaidieni tuupate ukweli toka katika matendo yenu na kauli zenu.