CC na Wabunge wa CCM Kipi ni Kipi....??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CC na Wabunge wa CCM Kipi ni Kipi....???

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwita Matteo, Aug 3, 2011.

 1. Mwita Matteo

  Mwita Matteo JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2011
  Joined: May 16, 2010
  Messages: 216
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Chama chochote makini huongozwa na Sera, sera kama dira hukiongoza chama katika kufikia malengo kilio jipangia na malengo mahususi ya Chama chochote makini cha siasa duniani ni kuwaletea wananchi wake maendeleo. Wabunge makini ni wabunge wanaowatetea wananchi waliowapigikia kura.

  Wabunge wote ndani ya Bunge ni mazao ya vyama mbalimbali, nikimaanisha hakuna mbunge ndani ya Bunge asie na Chama na vyama husika huwa na sera zinavyo isimamia ili kuhakikisha maendeleo ya Taifa na wananchi kwa ujumla yanafikiwa.

  CCM kama vilivyo vyama vingine ina sera yake na mmoja ya watu wa kuitetea sera yake ni wabunge walioko bungeni, kwa sababu katika vikao mbalimbali vya chama walipewa maelekezo ya sera na jinsi ya kuhakikisha wanaitetea. Sasa pale wanapoenda Bungeni na kupitisha vitu kwa asilimia mia kwa mia then kamati kuu CC inapokuja na kupinga maamuzi ya wabunge wa CCM, mi kidogo naona kuna tatizo hapa tena tatizo lenyewe ni kubwa. kuna mgongano ndani ya CCM kiasi hata Mbuge hajui yeye ni nani, Chama ni nini, Sera ni nini, Malengo na Matarajio ya Taifa ni Yapi.

  Hivi leo hii Mbunge wa CCM aliesifia kupandishwa kwa kodi ya mafuta taa ili kuzuia uchakachuaji anajisikiaje pale CC inapoamua kufanya kazi ambayo angeifanya yeye Bungeni?

  Hivi zile kejeli walizozitoa kwa kambi ya Upinzani walipo wasilisha bajeti yao Mbadala ilyolenga kuwapunguzia hali ngumu watanzania ambayo kwa kiasi kikubwa sasa inarejewa na CC, wanafikiri zilikua za kweli au sasa wao (CCM) ndio wanaihitaji sasa kuzodolewa na kuzomewa kwakuwa wameshindwa kuibana serikali na sasa CC imeamua kuchukua jukumu hilo.

  Mi nitoe rai, si lazima Mbunge uongee, kutetea uovu, dhuluma na ukandamizaji serikali inaoufanya dhidi ya wananchi na kikubwa Mbunge si msemaji wa Chama chama chake kwa sababu wasemaji wapo, nawe Mbunge vilevile si msemaji wa Serikali kwa sababu mawaziri wapo.

  Wabunge wa CCM mkiendelea hivi kila kukicha mtakua mnaibika, na itafika mahala sasa mtakua mnashindwa kutembea barabarani, kwasababu tutawazomea, unganeni Bungeni ili muibane serikali barabara na maendeleo ya patikane.

  Miaka 50 baada ya uhuru hatukupaswa kuwa hapa bali mbele zaidi

  Nawasilisha
   
Loading...