figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,487
Leo Tarehe 12/05/2017..kwa Mara ya kwanza nimepata nafasi ya kuchangia kwenye bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji. Nimegusia sehemu kubwa ya Wilaya ya Serengeti na kwa namna palivyo na uhaba wa upatikanaji maji hasa kwa Mji wa Mugumu na kata zake 7.
Lakini pia kwa eneo lote la Wilaya ya Serengeti kwa ujumla.
Nimesikitishwa kuona kwamba Serikali imetenga kiasi cha Tsh 850,000,000 pekee kwa bajeti ya mwaka 2017-2018 kwa mahitaji yote kwa Wilaya ya Serengeti, maana yake, hii igawanywe katika kila sekta ya kiamaendeleo kwa Wilaya, ambayo ni ukweli kuwa haitoshi kwa lolote.
Hivyo basi kwa mujibu wa Sensa ya mwaka 2012 Serengeti ina jumla ya wakazi 47,000 na Mugumu pekee ina Kata 7, na kuna bwawa moja tu kama chanzo cha maji(bwawa la Manchira) hivyo kwa namna yoyote ile miundo mbinu ya upatikanaji maji bado haijitoshelezi.
Lakini pia nimeelezea kwa namna ipi idara ya maji Mugumu (MUGUWASA)inavyojiendesha kwa hasara, kwa kuzingatia gharama kubwa ya uendeshaji mitambo na makusanyo ya kila mwezi kutoka kwa Wateja ambayo ni 7milioni tu, wakati MUGUWASA inalipia gharama za uendeshaji TANESCO takribani Milioni 16 kwa mwezi. Hivyo nimeiomba serikali kutafuta njia mbadala ya uendeshaji mitambo ya maji kwa Mugumu ili isaidie kupunguza gharama kwa shirika na kwa watumiaji pia.
Kingine nimeiomba serikali kuharakisha mchakato wa upatikanaji meter za maji kwa wakazi/wateja wa MUGUWASA kwa kuzingatia uwiano wa meter zilizopo na idadi ya wateja. Mathalani kwa sasa MUGUWASA ina wateja 1536 lakini ni wateja 509 tu waliounganishiwa meter za maji.
Kwanini nimeomba meter ni kwasababu tutaondoa urasimu mkubwa wa ufujaji wa pesa zetu na hii itaongeza pato kwa serikali.
Ahsanteni na nawakaribisheni kwa mawazo yenu.
Mungu awabariki sana.