Nipe Maji
JF-Expert Member
- Mar 25, 2025
- 335
- 190
Mbunge wa Viti Maalum kupitia Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Catherine Magige, amechangia sare 1,300 zenye thamani ya shilingi milioni 35.1 kwa wajumbe wa Baraza la UWT Mkoa wa Arusha.
Magige alikabidhi sare hizo mbele ya wajumbe wa baraza hilo lililofanyika mkoani Arusha, wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli zake kwa kipindi cha miaka mitano akiwa mjumbe wa Baraza la UWT mkoani humo.
Magige alisema mchango huo ni sehemu ya dhamira yake ya kuendelea kuwaunga mkono wanawake na kuimarisha mshikamano ndani ya jumuiya hiyo muhimu ya chama. Alieleza kuwa sare hizo zitasaidia kuongeza morali na mshikamano miongoni mwa wajumbe, hasa katika shughuli mbalimbali za kisiasa na kijamii.
Wajumbe walioshiriki Baraza hilo walipokea kwa furaha mchango huo, wakimpongeza Magige kwa moyo wa kujitoa na mchango wake mkubwa katika maendeleo ya jumuiya hiyo kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.