Card mpya za vyombo vya moto ni changamoto

Card mpya za vyombo vya moto ni changamoto

jerryempire

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2017
Posts
5,830
Reaction score
10,091
Habari,
Nikiwa kama mdau wa kuuza na kununua magari used na mapya kutoka japan imenibidi leo ni share hili jambo la card mpya zinazotolewa na TRA kwa sasa.

Kadi za mwanzo zilikuwa ni hard copy,card ambayo imetenge ezwa kwa material na kuwekwa seal maalum ambazo sisi kama (car dealer's),ilikuwa ni rahisi kugundua kama card hii ni original ama feki.

Ila mfumo wa sasa wa card hizi mpya mtu endapo kama mtu ataiiba soft copy ya card yako na ukamuazima chombo chako basi jua anaweza kwenda kukiuza pasipo wewe muhusika kujua endapo mnunuzi hatambui hatua za kufanya pindi anunuapo chombo hicho.

Japo kwa sasa tunahakiki card kupitia namba za simu za mhusika endapo majina yanaendana ya kwenye card na kwenye vitambulisho lakini hii imekuwa changamoto kwetu hasa kwa siku za weekend sababu kunawakati unakuta mtu amesajilia line ambayo haina majina yake halisi hivyo unashindwa kufanya biashara ama biashara kuhairishwa.

TRA,mnapaswa kuliangalia hili kwani card zenu mpya zinatoa mianya mingi ya watu kufanya uhalifu, uhalifu ambao mwisho wa siku huumiza watu wengi ambao wengine hawakuwa hata na hatia.

Gari inaibiwaje?
Hizi card mpya zinakuwa na mfumo wa bar code ambayo ukiiscan na simu yako inakupa taarifa za gari husika kama mwaka,aina ya gari,jina la mmiliki n.k?

Card hii inakuwa katika mfumo wa karatasi, yeah karatasi hizi hizi za kawaida A4, au unaweza kuihifadhi katika email au hata kwenye whatsapp yako na unaweza kuishare kwa mtu unayetaka kumuuzia gari yako japo wewe ndie utahekuwa na uwezo wa kufanya transfer kwenda kwa unaemuuzia.

UNAWEZAJE KUIBIWA?
Hii ni njia moja nyingine sitozitaja kuepusha wengine kuzitumia vibaya kwenye uhalifu huu.

1: anaweza kutokea mtu wako wa karibu jamaa ama rafiki akapata access ya kuishika simu yako na kwenda kwenye email ama whatsapp maana wengi wetu huwa tunatumia ma agent kwenye issue za transfer, Hivyo basi endapo atafanikiwa kupata copy ya card ya gari yako anauwezl kwenda kuiuza kwa mtu na huyo mtu punde aonapo card hyo na kuiscan bar code na kuonyesha ni card original bas biashara hufanyika pasipo wewe kujua,

Nini hufanyaga kuhakiki,
Sisi kama car dealer's hukagua card hyo kama ni fake ama original kwa kuscan bar code lakini pia huhakiki vitambulisho kama majina ya kwenye vitambulisho na kwenye card yanaendana lakini mwishoni huchukua namba za simu hizo na kuzihakiki majina kama yanaendana kwenye vitambulisho na card na mwishoni hupigiwa muhusika kama ameridhia kuiuza gari hyo endapo aliyeleta anayeuza gari hyo jina lake halisomi.

Endapo mhusika hapatikani,na majina ya kwenye simu ni tofauti na kwenye card hapo uamuzi wa kwenda TRA hufanyika kwa ajili ya uhakiki jambo ambalo hufanya biashara kuwa ngumu kwa siku za weekend sababu TRA huwa hawafungui.

Wengi ambao hawajui kuhakiki card hizo wamejikuta wakiuziwa magari ya wizi na mwishoni kuishia kwenye matatizo.

Hali hii imetufanya tufanye biashara kwa makini mno kiasi cha kwamba kuna magari hatununui na kuna magari unampeleka mteja kabisa analipenda lakini zikija document's inabidi kama dalali uvunje biashara sababu endapo utaiuza hivyo hvyo kimazabe matatizo yakija yanaanza na wewe kwanza.

Nikiwa kama mdau wa kuuza na kununua vyombo vya moto tunaiomba serikali yetu kuliangalia hili kwa makini na kulichukulia hatua upande wa card tu

KWA MAHITAJI YA KUUZA NA KUFANYA TOP UP AU KUNUNUA GARI YAKO AMA KUSAFIRISHA GARI YAKO KARIBU UWASILIANE NAMI NIKUHUDUMIE KWA HARAKA NA UAMINIFU MKUBWA TUNAPATIKANA DAR ES SALAAM. 0740092929 CALLS/WHATSAPP
 
Attachments

  • images (20).jpeg
    images (20).jpeg
    31.4 KB · Views: 21
Habari,
Nikiwa kama mdau wa kuuza na kununua magari used na mapya kutoka japan imenibidi leo ni share hili jambo la card mpya zinazotolewa na TRA kwa sasa.

Kadi za mwanzo zilikuwa ni hard copy,card ambayo imetenge ezwa kwa material na kuwekwa seal maalum ambazo sisi kama (car dealer's),ilikuwa ni rahisi kugundua kama card hii ni original ama feki.

Ila mfumo wa sasa wa card hizi mpya mtu endapo kama mtu ataiiba soft copy ya card yako na ukamuazima chombo chako basi jua anaweza kwenda kukiuza pasipo wewe muhusika kujua endapo mnunuzi hatambui hatua za kufanya pindi anunuapo chombo hicho.

Japo kwa sasa tunahakiki card kupitia namba za simu za mhusika endapo majina yanaendana ya kwenye card na kwenye vitambulisho lakini hii imekuwa changamoto kwetu hasa kwa siku za weekend sababu kunawakati unakuta mtu amesajilia line ambayo haina majina yake halisi hivyo unashindwa kufanya biashara ama biashara kuhairishwa.

TRA,mnapaswa kuliangalia hili kwani card zenu mpya zinatoa mianya mingi ya watu kufanya uhalifu, uhalifu ambao mwisho wa siku huumiza watu wengi ambao wengine hawakuwa hata na hatia.
Ungeweka walau sample ili ieleweke, siyo wote tumeziona hizo kadi mpya.
 
Muhimu hapa, ni mnunuzi alipie baada ya kubadili jina la kadi na kusoma jina lake kwenye mfumo.
 
Muhimu hapa, ni mnunuzi alipie baada ya kubadili jina la kadi na kusoma jina lake kwenye mfumo.
Siyo solution, wewe unaweza kubali mtu alipe 250k kwa ajili ya kubadili gari yako kwenda kwenye jina lake na gari yako inathamani ya 50m?

Once akishachange jina gari inakuwa ya nani? Wakati huo umelipwa bei gani?
 
Iwe imejieleza kwenye mkataba, ni sawa na kulipia gari japani wakati gari bado hujapokea.
 
Mkuu, huu mfumo ni salama kuliko ule wa hard copy, we sema imepunguza usalama wa kuuza gari kwa niaba. Kipindi cha hard copy hata anayeuza hamjui anayesoma jina kwenye card maana na yeye aliuziwa na ambaye hakubadili jina, as long as card ni OG na kuna id na passport biashara inafanyika.

Serikali iboreshe, iwape wanasheria, mawakala access ya kufanya transfer badala ya portal ambazo raia hawajui, haya yafanyike wakati wa kuandikishana mikataba. Kuna pesa nyingi mno kwenye biashara ya magari serikali haizioni.
 
Juzi nilikua ninauza gari almanusura biashara ife kisa hayo mambo ya kadi.

Jamaa alikua tayari kishalipa hela, kuja kucheki na mhusika mwenye jina kwenye kadi(gari ilishauzwa mara nyingi na watu walikua hawabadili umiliki)anasema hiyo gari siijui.

Mnunuzi akachukua hela yake fasta, ikabidi itumike akili na nguvu ya ziada kumrudisha kwenye mstari.
 
Pole sana mkuu mie mara kibao zinakufa unakuta card na vitambulisho vinasoma jamali lakini namba ya simu inasoma fatuma na ukimpigia simu fatuma hapokei au hapatikani so hapo uchaguzi unakua
 
Back
Top Bottom