Mad Max
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 31,139
- 88,801
Wakuu, kwema?
Leo tuongelee hizi Spark plug na coils ambavyo ni vitu vya muhimu sana kwenye gari, na ndiyo zinazoamua kama engine yako irun smooth au rough wakati wa utendaji wa kazi.
Hivi viwili visipobadirishwa kwa wakati, gari linaanza kumiss (ile milio ya puh puh puh), rough hidle, kutumia mafuta vibaya, na kushindwa kupanda milima sana sana ukiwa speed ndogo.
SPARK PLUGS
Spark plugs zinatoa cheche (spark) inayowasha mchanganyiko wa hewa na mafuta ndani ya kila cylinder.
Kila spark inayotokea, (approximately mara elfu moja kwa kila sekunde,) ndio inayopelekea engine iendelee kuwaka.
Aina za Spark Plugs:
Aina kuu za spark plugs ni tatu, na zinatofautiana kutegemeana na uimara, lifespan, design, gharama na performance:
1 Copper (zinc-coated) hizi bei zake ni rahisi, inadumu km 15,000–25,000
2 Platinum: hii inadumu kwa 50,000–80,000 km
3 Iridium: za kisasa zaidi, hudumu hadi 100,000–120,000 km
(hizi ndizo zinazotumika kwenye magari mengi ya kisasa mfano Toyota, Honda, Mazda, Suzuki, n.k.)
Mifano ya common spark plugs tunazokutana nazo madukani hapa bongo:
• NGK Iridium IX hizi maarufu sana (bei 25k–45k Tsh kila moja)
• Denso Iridium TT original za Toyota na Lexus.
• Bosch Platinum – kwa magari ya Ulaya (BMW, VW, Benz)
• Champion inatumika kwenye baadhi ya Nissan, Mazda.
Dalili za Spark Plugs zilizochoka:
• Gari lina “misfire” (engine inatetemeka au inakata kata unaweza hisi mafuta yameisha, tena sana sana ukiwa speed ndogo au parking)
• Matumizi ya mafuta kuongezeka ghafla
• Kuchelewa kuwaka (starting delay) tena sana sana cold start za asubuhi
• Exhaust kutoa moshi mweusi au harufu ya mafuta
• Check Engine Light kuwaka (mara nyingi inatoa DCT P0300–P0304)
Interval ya Kubadilisha:
Kutegemea na matumizi yako na aina ya spark plugs ulizoweka, interval ya kubadirisha itatofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine. Mfano:
• Iridium zinaweza kwenda 80,000 hadi 100,000 km
• Platinum zinaweza kwenda 50,000 km
• Copper kuanzia 20,000 km
Kwa Tanzania (baridi kidogo na vumbi), ni vizuri kubadilisha kabla ya kufika maximum recommended distance au ukianza kuona dalili ata mapema.
Tips za Wakati wa Kubadilisha:
• Jitahidi ubadirishe zote kwa pamoja (kila cylinder). Either 3, 4 au 6 kutegemea na gari lako.
• Usichanganye aina tofauti za plugs kwenye engine moja
• Hakikisha “gap” ipo sahihi kama ilivyo kwenye manual (0.8 hadi 1.1mm kwa magari mengi), kama hauna uhakika baadhi ya maduka ukitaja engine code ya gari lako wanasearch wanakupa plug sahihi, mfano Toyota Kariakoo.
• Tumia original brands, feki zipo nyingi sana mjini, ni bora ununue maduka yanayoeleweka.
• Usifunge kwa nguvu sana, unaweza kuvunja thread kwenye head au kama vipi muachie tu fundi akubadirishie. Haizidi buku 20 hela ya ufundi.
IGNITION COILS
Ignition coil ni kama transformer ndogo inayogeuza umeme mdogo kutoka kwenye battery (12V) kuwa umeme mkubwa zaidi (hadi 30,000 volts), ili kuzalisha cheche kwenye spark plug.
Kila cylinder ina coil moja (kwa magari ya kisasa), au moja inashare kwa silinda kadhaa (kwa magari ya zamani).
Aina Kuu:
Zipo nyingi ila tatu kuu naweza ziandika kutoka kwenye mchoro hapo juu:
1 Coil-on-Plug (COP) hizi coil moja moja juu ya kila plug (common kwenye Toyota, Honda, Nissan za kisasa).
2 Distributor Coil na Wasted Spark hizi coil moja inasambaza cheche kwa silinda kadhaa (magari ya zamani).
Dalili za Coil Iliyochakaa:
• Injini inamiss au inatetemeka, inakua kwa nguvu zaidi ya ile kwenye spark plugs, especially ukiwa umepark au speed ndogo.
• Check Engine Light inawaka unavyozidi kutumia (mostly inaleta DTC P030x)
• Gari kupoteza nguvu, ina acceleration ndogo, na mlimani haipandi kabisa.
• Moshi mweusi au harufu ya mafuta kwenye exhaust
• Wakati mwingine gari linaweza ku-stall ghafla (kama imeishiwa mafuta hadi uwashe tena)
Bei za Coils:
Uzuri coil haina haja ya kubadirisha zote, mara nyingi unatakiwa ujue ni ipi yenye shida na kuibadirisha. Bei zake kidogo sio rafiki, kwa Japanese nyingi ni Tsh Elfu 70 hadi Tsh 150k, ila zipo ata za zaidi.
Kwa gari za ulaya, kidogo za moto zaidi. Mara nyingi bila 180k kupata ngumu.
Tips Muhimu za Coils:
• Siku ukibadirisha plug, kagua coil pia (angalia kama kuna mafuta au kutu juu yake).
• Usioshe coil kwa maji, itaharibu windings ndani.
• Tumia coils originals tu (Mfano Denso, NGK, Bosch, Hitachi, Delphi), feki zinachakaa mapema au hazifanyi kazi ipasavyo. Tumewahi agiza za kichina kwa Elfu 50 each kwaajili ya BMW zilikua 6, aisee Mchina hafai. Zilikua za kutupa tu.
Kwa leo tuishie hapa wakuu. Pamoja.