Can you do it

omary2222

Member
Joined
Jun 18, 2012
Posts
78
Reaction score
25
[h=5]Kijana asiye na kazi aitwaye Nolesy aliamua kumwoa rafiki yake wa muda mrefu aliyekuwa akifanya kazi katika benki moja mashuhuri.

Nolesy alijitosa katika ndoa licha ya hofu na ushauri mwingi aliopewa na ndugu kuwa ni vibaya kuoa ukiwa huna kazi.

Kila mwezi yule binti alimpa mmewe mshahara wake wote wa 800,000 baada ya kutoa fungu la kumi kwa ajili ya kanisani.

Nolesy yeye alitoa 200,000 na kumpa mkewe kwa ajili ya matumizi binafsi na zilizobaki kijana aliamua atumie kwa matumizi gani. Na hali hiyo ilidumu kwa miaka mitatu mfululizo.

Furaha na amani viliitawala nyumba ile na kwa wanandoa wale pia kwa miaka mitatu pamoja na kuwa marafiki wengi wa yule dada walimfuata na kumwambia huwezi ukawa unalipa bill zote za nyumba na kufanya kazi zote wewe tuu na mmeo kakaa tuu kwa nini msiachane?

Kuna mwezi mmoja kijana yule alitumia zaidi ya 500,000 akizunguka mikoa mbalimbali kwa ajili ya intavyuu za kazi.

Hatimaye kijana alifanikiwa kupata kazi Mbeya katika kampuni ya Green Entertainments na kuwa meneja mkuu huku akipokea mshahara wa milioni tatu na nusu kama kianzio.

Akanunua gari yake ya kwanza mpyaa kwa bei ya shilingi 18M na akampa funguo mkewe na kuendelea kutumia usafiri wa daladala kwa zaidi ya miaka miwili.

Baada ya hapo akanunua gari la pili jipya lenye thamani ya 30M na kumpa mkewe na kulichukua gari la zamani na kulitumia yeye na mpya kumpa mkewe.Miaka michache baadae wakahamia kwenye nyumba yao.

Siku moja mke alikuwa akitafuta dokyumenti zake katika makabrasha mbalimbali pale chumbani kwao, alishangazwa kuona kuna bahasha ndogo imefichwa na ndani kuna picha yake wakati wa harusi na akaona kuna dokyumenti nyingine za manunuzi kiwanja na magari na vyote vikiwa vimeandikwa kwa jina lake kabla ya kuona maandishi yaliyoandikwa:

''MKE WANGU NI KILA KITU KWANGU. ALIKUBALI KUOLEWA NA MIMI NIKIWA SINA KITU, NA SASA NAAMINI HATA NIKIWA NA VITU VYOTE NI VYAKE KWANI MOYO WAKE NI ZAIDI YA KILA KITU KWANGU NA FAMILIA YETU.AISHI MILELE"

Machozi yalimtoka dada yule na alifurahia sana ujumbe ule kabla ya kukumbuka kuwa wiki chache baadae ilikuwa ni kumbukumbu ya miaka yao ya ndoa.

Hivi sasa MUNGU amewabariki na wana watoto wawili wakike na wakiume na wanapendana mara mia zaidi ya mwanzo.

Jamani mapenzi ya kweli yapo mpaka sasa.

Je una uhakika kuwa mapenzi uliyonayo kwa mwenza wako ni sawa au yanaweza kulinganishwa na haya?

Pamoja na vyote lakini kumbuka mnachaguana ili kuishi kwa shida na raha na haijalishi nani ananunua mahitaji ya nyumbani au kulipa bili kwa sasa.........[/h]
 
Habari za kusadikika hizi, hamna lolote. Hawa dot com hawa..
 
hapo ndipo utamu wa mapenzi ulipo
 
wewe ni zaidi ya shigongo..
 
Aisee ya kweli hayo? I wish namiye nimpate wa hvyo!! Loh

utamtoa wapiiiiiiiiiiiii. khaaaaaaaaaaaa eti akuhudumie three years then wanaume wenyewe majanga wakishafanikiwa hawachelewi kutafuta nyumba ndogo
 
blah blah blah. Mshahara wa milioni tatu na nusu, na hizo laki nane za mke ndio zinanua vitu hovyo hovyo hivyo??? BOra ungeweka mshahara wa milioni 20.

Pili dokyumenti sio kiswahili, kiswahili sanifu ni waraka na wingi wake ni nyaraka.
 
That TYPE OF ORGANISM IS EXTINCT!!!!!!!!!!!!!!!! Not even DORMANT! Siku hizi hata ukikuta PICHU ina jina lako unashuruje!!!!!??????? Tena ukiw zoba vyako anaviuza mchana kweupeeeeeee!
 
utamtoa wapiiiiiiiiiiiii. khaaaaaaaaaaaa eti akuhudumie three years then wanaume wenyewe majanga wakishafanikiwa hawachelewi kutafuta nyumba ndogo

sio wote ni majanga samaki mmoja akioza mtoe mtupe
 
Mhhh hyo stori imenigusa jmn,lakini bahati ya mwenzio usilalie mlango wazo
 
Hii story nimeiona kwenye page moja inaitwa sex and relationship in afrika...sasa mtoa mada alichofanya ni kuitafsiri tu kwa kiswahili....ila mkuu we mbayaaaaaaaaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…