Can Democracy and Development be pursued by ignoring the local cultures?

Attache

Senior Member
Jul 6, 2012
175
147
Kumekua na maneno mengi kuwa demokrasia ya Africa ima-fail na wengine ku-mock kuwa demokrasia imetushinda wa Africa na hivyo tugeukie mpira.

Swali ni kwamba where did we go wrong? Ni kweli Demokrasia imetushinda au ni kwamba kuna namna ambayo tunaweza ku Africanize political systems na ku-come up na ile ambayo ita fit context yetu?
 
Mkuu tukiichukilia maana halisi ya demokrasia kama ni utawala wa waliowengi (majority rule) basi itakuwa kwa kweli Afrika tumefeli kabisa katika kutekeleza hio demokrasia. Mfano mzuri wa kufeli kwa demokrasia ya utawala wa waliowengi basi tunao hapa hapa kwetu Tanzania. Katiba ya Tanzania inasema wazi ya kwamba uongozi wa nchi hii huchaguliwa kila baada ya miaka 5 kwa utaratibu wa kura wa mtindo wa wengi wape. Katika uchaguzi wa Zanzibar wa 2015 kuna uthibitisho usio na shaka yoyote ya kwamba wengi wa wapiga kura wa Zanzibar walichagua viongozi ambao ni tofauti na mapenzi ya watawala. Lakini kwa vile Tanzania hatuna demokrasia basi tuna maigizo ama usanii wa demokrasia, matokeo yake ni kwamba maamuzi ya waliowengi yamepuuzwa na kufutwa kabisa. Bado hatujui kama tutavuka salama hapa au laa? Hii inathibitisha ya kwamba ile majority rule haina maana yoyote mbele ya watawala hata kama wao ni wachache. Ili Kuondoa huu usanii wa demokrasia basi mimi ningeshauri ni bora tukarudia uongozi wetu wa Afrika wa asili. Ni bora tukarudia enzi zile za Machifu, watemi na Mamwinyi kutawala. . Mbona bado kuna baadhi ya nchi katika bara hili la Afrika zinaendelea na utaratibu huo na wala hakuna mikwaruzano yoyote. Nchi kama Lesotho na Swaziland kama sikosei bado zinaendelea na utaratibu huo wa kiasili. Ni afadhali ya kurejesha utawala wa chifu wa kizanaki au mkwawa au watemi kuliko kuendelea na usanii huu wa Demokrasia hapa kwetu Tanzania.
 
Mkuu Point yako nimeielewa sana, pia nitapenda kuizungumzia nikiwa vizuri
 
Back
Top Bottom