Ulitaka wasafari kwenye mikokoteni?
Ulitaka wasafari kwenye mikokoteni?
Kisheria hairuhusiwi kubeba watu kwenye lorry nyuma(ambayo ni sehemu ya mizigo) wala kwenye pickup kwa nyuma.Lakini kama ujuavyo,CCM iko juu ya sheria za nchi hii.Na ikitokea ajli wakafa,itakuwa kazi ya Mola manake ndo anayeendesha malori.
Ulitaka wasafari kwenye mikokoteni?
Malkia Marie Antoinette wa Ufaransa alishawahi kuwa na majibu kama hayo. Kuna wakati wa miaka kama sikosei ya 1700, wafaransa walipatwa na njaa. Wakamfuata mfalme wao kumuomba mikate. Huyo malkia aliposikia wananchi wanaomba mikate, akashangaa na kusema, 'Kama hawana mikate, kwa nini wasile keki?' Wananchi hawakusahau majibu yake, na mara baada ya mapinduzi, yeye pamoja na mfalme walikatwa vichwa hadharani. Ole wenu nyie mnaowabeza wananchi...hukumu yao kali!Kibunango, tunajua familia yenu iko ccm tokea enzi, kuna mambo ambayo hutakiwi kutetea, kupanda roli unaona ni sawa? Endelea kutetea ufisadi mzee, hatukuzuii. Ila siku moja watu wataingia msituni japo si leo.
Ulitaka wasafari kwenye mikokoteni?
Mkuu naona unazungumzia zaidi CCM kabla ya vyama vingi, ambapo wananchi hawakuwa na chaguo la chama zaidi ya CCM. Sasa ni wakati mwingine na sidhani hayo ya kale kama yataweza kurudi chini ya CCM au Chama kingine chochote katika mfumo kama huu.uzalendo uliokuwapo CCM ambapo watu walienda kwenye mikutano hadhara kwa usafiri wao...,walitembea maili kadhaa ....watu walifanya kazi za kujitolea wakachimba barabara,wakajenga viwanja vya michezo kote nchini kama sheik amri abeid,kirumba,jamhuri,samora,vita,..uliishia kwa kujenga uwanja wa ALI HASSAN MWINYI TABORA...ambavyo leo hii hadi serikali itenge budget...hiyo ndio CCM wengi tuliokuwa nayo ...tukiimba halaiki na kucheza magwaride ....bila kuppewa chochote....siku hizi hata mahalaiki watoto hawaendi mazoezini hadi walipwe effu 2,000 kwa siku.....huku hazina ikiambiwa wanalipwa elfu 5,000 kwa siku.....tunaelekewa wapi???
Malkia Marie Antoinette wa Ufaransa alishawahi kuwa na majibu kama hayo. Kuna wakati wa miaka kama sikosei ya 1700, wafaransa walipatwa na njaa. Wakamfuata mfalme wao kumuomba mikate. Huyo malkia aliposikia wananchi wanaomba mikate, akashangaa na kusema, 'Kama hawana mikate, kwa nini wasile keki?' Wananchi hawakusahau majibu yake, na mara baada ya mapinduzi, yeye pamoja na mfalme walikatwa vichwa hadharani. Ole wenu nyie mnaowabeza wananchi...hukumu yao kali!
waungwana niko Mtwara leo, na kama nusu saa iliopita nikiwa kituoni nasubiri dala dala niendelee na mizunguko yangu, yamepita maroli yanawarudisha wana CCM majumbani mwao, kutoka kwenye campaign.Katika kampaign hizo ambazo sikupata bahati ya kuhudhuria ninaambiwa kulikuwa na kikundi cha ze comedy katika kuongeza idadi ya wahudhuriaji. Point kubwa iliyonifanya nilaunch hii thread ni usalama wa hawa watu wanaojazwa kwenye haya maroli.Usalama wao unaangaliwa kwa umakini kweli hasa ukizingatia yale magari hayajawa designed kubeba watu? Pia nataka mnisadie kujua kama sheria inaruhusu kujaza watu vile kwenye maroli? Naombeni wana JF tuliangalie hili limekaaje hasa ukizingatia kipindi hichi tumekuwa tukiripotiwa habari nyingi sana zinazohusu ajali za
barabarani hapa TZ.
hakuna sheria yoyote ya usalama barabarani inayoruhusu kupakia abiria kwenye maroli isipokuwa kwa kibari maalum lkn najua ccm hutumia ubabe kuwasafirisha subiri mabaya yakitokea (ingawa siombei iwe hivo mungu epushia mbali)