bluetooth23
JF-Expert Member
- Apr 8, 2013
- 348
- 326
Camp Mulla ni kundi la afro hip hop kutoka Nairobi Kenya lililoibuka mwaka 2010 na kujizolea mashabiki lukuki ndani na nje ya Africa. Walipata kuwa nominee kwny BET, MTV Europe, Kora Africa na awards nyingne nyingi. Ngoma zao kwa uchache tu ni kama Addicted, party dont stop, fresh all day, na prices waliyoigonga na mkali kutoka Nigeria Wizkid. Hivi tunavyoongea Camp Mulla hawapo pamoja tena, wasanii wamesambaratika na kundi limebak na waasisi wawili tu huku Shapperman na Mwanadada Miss Karun wakitimkia USA kupiga shule University, naye producer wao K"cous wa Sub Saharan Records akiwafuta lebo waliobakia. Na hata director wao wa video bwana mdogo Andrew 'Andy' Mancharia aliyedirect video ya Fresh All Day naye akitimikia Los Angeles USA alikokulia na kusomea. Kuna taarifa zisizo rasmi kuwa mwanadada Tiri na mkali Collo wanatarajiwa kuwa usajili mpya kuunda upya Camp Mulla itakayokuwa chini ya usimamizi wa karibu wa tajiri CMB Prezzo ambaye hata awali alikuwa sapota mkubwa wa ile real Camp Mulla...