Travelogue_tz
JF-Expert Member
- Sep 28, 2010
- 855
- 1,224
MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, amesema hafanyi kazi kwa msukumo ama amri zinazotolewa na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), likiwamo suala la ukaguzi wa tuhuma za miradi ya ufisadi zinazomkabili Meya wa Manispaa ya Bukoba, Anatory Amani. Utouh amesema kuwa si kweli kwamba ameagizwa na Rais Jakaya Kikwete, Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi wala Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, kwenda kufanya ukaguzi mkoani humo.
Mimi nimeombwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kukagua hesabu za manispaa hiyo na ninakanusha madai kuwa Nape ameniagiza, alisema CAG muda mfupi baada ya kufungua warsha ya wahariri wa habari na asasi za kiraia iliyoandaliwa na ofisi yake jana.
Utouh alisema kuwa rais hahusiki na ukaguzi huo, wala hajauomba yeye, hivyo si kweli kwamba amekaidi agizo lake.
Kauli ya Utouh inakinzana na tamko la kisiasa la CCM kwa umma lililotolewa kupitia Nape, kwamba kamati kuu ya chama hicho ilimuagiza mkaguzi huyo kwenda Bukoba ndani ya wiki moja kuanzia Agosti 27, mwaka huu kufanya ukaguzi wa tuhuma hizo.
Utouh alisema kuwa Nape anahusika na chama, wanasimamia fedha na mali za chama, wakati Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali inasimamia mali na fedha za umma, hivyo akahoji ni kwa mamlaka gani Nape anaweza kumuagiza.
Alisema kuwa wao ndio wataalamu wa kujua uzito wa hiyo kazi na wanavyotaka ifanyike, kwa hiyo wanapoombwa na kukubali hawabanwi na siku alizotaja mwombaji.
Ukaguzi wa Bukoba hatujauanza bado na naomba niwaelimishe kuhusu ukaguzi maalumu, ukaguzi maalumu unapoombwa si jukumu la yule aliyeomba kunipa siku za kufanya ukaguzi, kwa sababu anayeomba si mkaguzi, alisema.
Aliongeza kuwa hata baada ya kuletewa hadidu za rejea si lazima wazikubali, bali wanaangalia kama zinaendana na utaratibu mzima wa kufanya ukaguzi unaoendana na ule wa kimataifa.
Ninavyokwenda sasa hivi nawahakikishia kuwa baada ya majadiliano na waziri mkuu kuhusu hadidu za rejea, tuko kwenye mchakato wa kupanga kwenda Bukoba, nakwenda mwenyewe wiki ijayo kwa ajili ya kuwa na kikao, tunakiita cha kuingilia kabla ya ukaguzi, alisema Utouh.
Alisema kuwa kwa mujibu wa masharti ya ukaguzi maalumu kama huo, muombaji, yaani waziri mkuu atapaswa kumpatia hadidu za rejea, jambo ambalo linaendelea kufanyiwa kazi sasa kati ya pande hizo mbili.
Halafu kwa masharti hayo huyo anayetuomba hapaswi kutupangia muda wa kwenda kufanya kazi hiyo, alisema.
Kumekuwapo na malalamiko kwa baadhi ya wakazi wa Bukoba wakidai kuwa siku chache baada ya Kamati Kuu ya CCM kumwagiza CAG kufanya ukaguzi, mbinu mbalimbali zimekuwa zikifanywa na baadhi ya watendaji wa manispaa wasio waaminifu za kutaka kuficha nyaraka.
Baadhi ya watendaji hao wanadaiwa kukesha ofisini kwa siku mbili, jambo lililotafsiriwa kama mkakati wa kubadili nyaraka kabla CAG hajaanza ukaguzi.
Katika kumaliza mgogoro wa umeya mjini Bukoba, Kamati Kuu ya CCM ilitengua uamuzi wa kuwafukuza madiwani wanane wa manispaa hiyo, ikidai kuwa Halmashauri Kuu ya Mkoa wa Kagera iliyokuwa imewafukuza ilikiuka katiba.
Kamati hiyo ilimwagiza CAG kwenda mjini Bukoba kukagua tuhuma hizo dhidi ya meya, kisha ripoti hiyo kuwasilishwa kwenye Baraza la Madiwani ili hatua zaidi zichukuliwe kama ikithibitika alifanya ufisadi.
Katika kikao hicho, Rais Jakaya Kikwete alikiri timu iliyoundwa na waziri mkuu kuchunguza mgogoro huo kuwa ilibaini mianya ya ufisadi katika manispaa hiyo.
Baada ya ukaguzi huo, madiwani wanaweza kufanya lolote wanalotaka. Kama ni kumfukuza meya au la, wataamua wao.
Rais pia aliagiza viwanja 800 vilivyokuwa na mgogoro warudishiwe wananchi waliokuwa wanavimiliki na wasitozwe hata senti tano.
Madiwani hao wamekuwa wanamlalamikia meya kuwa ameiingiza manispaa katika ufisadi kwenye miradi kadhaa.
Miradi hiyo ni upimaji wa viwanja 5,000 unaodaiwa mkopo wake wa sh bilioni 2.9 kutoka Mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji (UTT) ambao haukufuata taratibu na wananchi hawakushirikishwa ipasavyo.
Tuhuma nyingine ni mradi wa ujenzi wa soko. Meya anadaiwa kusitisha malipo ya ushuru na kutaka kuwaondoa wafanyabiashara bila kufuata utaratibu.
Anatuhumiwa pia kukopa sh milioni 200 kutoka Benki ya Uwekezaji (TIB) bila kibali cha Baraza la Madiwani.
Vilevile alitoa taarifa kwenye kikao cha baraza hilo kuwa TIB iliwapa ruzuku ya sh milioni 90, lakini hakueleza misingi yake.
Upo pia mradi wa kuosha magari ambao unadaiwa kutumia kiasi cha sh milioni 297 zinazotiliwa shaka.
Ameshindwa pia kutoa mchanganuo wa mapato na matumizi ya mradi ya kiasi cha sh milioni 134 za ujenzi wa kituo cha mabasi.
Katika hatua nyingine, Utouh amesema kuwa kuna upotoshaji mkubwa wa taarifa za ukaguzi anazotoa katika ripoti mbalimbali nchini.
Utouh alisema baadhi wamekuwa wakichapisha taarifa au habari ambazo zinapotosha umma na hata kuchochea machafuko yasiyo ya lazima.
Alisema kuwa uwajibikaji na uwazi ni mambo ambayo hayawezi kupatikana katika mfumo unaoendeleza ufichaji wa taarifa za utekelezaji wa mipango mbalimbali ya serikali.
Pale ambapo habari inafichwa lazima patatokea hali ya uvutano na kutoaminiana na hatimaye wananchi wataona serikali yao ndiyo inasababisha matatizo, alisema.
Alisema kuwa ni lazima kuelewa madhara ya kuripoti taarifa za upotoshaji na mipaka ya yale yanayohitajika kuripotiwa.
Tunahitaji kufikiria masuala mazito yanayokwamisha kufikia malengo yetu tujiulize tunawezaje kupunguza utoaji wa taarifa zisizo sahihi ili kuboresha mahusiano yetu na uwezo wa kupata habari sahihi za serikali, alisisitiza Utouh.
Tanzania Daima
Ifuatayo ni sehemu ya Tamko la kamati Kuu ya CCM kuhusu Meya wa Bukoba kupitia kwa Nape Nnauye, soma hapa
mjengwablog.com/habari-za-kijamii/item/5008-ccm-yamwagiza-cag-kumchunguza-meya-bukoba.html#.UkKs0n87