Cag report and social security funds

mwenzetumwenzetu

New Member
May 30, 2012
4
3
Nasikia haya mashirika yana pesa nyingi za kutisha lakini jinsi fedha zinavyowekezwa mashaka lazima yatande kila mahala. naomba kuuliza yafuatayo.

1. Hivi hiyo Riba tunayopata ya kama asilimi 0.005 inatusaidia nini wakati inflation rate ni kubwa? Wao wanasema faida ni kubwa, yaani ukiwekeza tusema billion 30 basi sio zaidi ya miaka 5 utakuwa umerudisha mtaji. Mbona pesa zetu haziongezeki kiasi hicho? Mimi niliweka Tshs, 20m miaka zaidi ya 10 iliyopita lakini nimekuta ninaongezeko lisilozidi laki 3 kwa miaka yote hiyo. Hii pesa kama ningenunua mashamba miaka 5 iliyopita leo ungekuta nina zaidi ya million mia. Hivi haya mashirikia ya hifadhi za jamiii yanatusaidia au yanatuibia mchana kweupe?
2. ili upewe pesa zako lazima umri wako usiwe chini ya miaka 55. Hivi umri wa kuishi wa mtanzania ni miaka mingapi?

3. Kwanini mtu anapoacha kazi na ukitaka mafao yako lazima tena urudi kwa mwajiri wako akujazie michango yako ya miaka yoooote, hivi kweli huu sio ukiritimba wa kutupwa? Kwani kunatatizo gani hii pesa inavyoingizwa kwenye akaunti yako na huyo mwajiri isichukuliwe kama vile pesa inaingia kwenye bank akaunti yako tena kuwe na ATM card na pia taarifa (Notification) kuwa pesa imeingia kwenye akaunti yako kila mwezi? hii michango ya kila mwezi inayopelekwe kwenye haya mashirika basi taarifa zitumwe moja kwa moja kwenye mtandao wa simu kuwa pesa yako imeingia kwenye akaunti yako ya mfuko wa jamii. Hii itasaidia sana watu kupata taarifa za michango yao na pia mwajiri atakuwa hadanganyi. na siku unapostaafu basi uwe unauwezo wa kujua kiasi kilichoko na pia hiyo kadi yako iwe kama vile ATM card, iwe enabled ili mteja aweza kuchukua pesa zake bila ya kusubiri msururu mrefu wa kujazia maform kwa maform kutoka kila kona, sehemu ambazo ulikwisha fanya kazi. Kwani kuna ubaya gani mtu akijua pesa inayoingia kwenye akaunti yake ya mfuko wa jamii kwa njia ya simu? Mwajiri akichelewa kupeleka pesa tu, basi lazima wafanyakazi wachachamae.

naomba kuwakilisha.
 
Naomba, tuambie hiyo pesa inayokaa kwenye haya mashirika ya kijamii, yanatulipa riba kiasi gani kila mwaka, kama wao wanapata mabillion?
 
Mkuu kitu ambacho huwa kinanitisha ni uhuru waliopewa viongozi wa mashirika haya ya hifadhi ya jamii!! Wanajiamulia wancho taka na sijuhi kuwekeza kwenya nyanja nyingine ambazo zinashangaza sana - hawawajibiki chochote kwa wafanyakazi wanao katwa fedha za hifadhi kwenye mishahara yao!

Wameweka a groud breaking Information Technology Systems kwenye mashirika hayo lakini wakasahau kuweka application program za kutoa taharifa kwa wanachama kupitia simu za mikononi pindi pesa inapoingia! Wanashindwa na Bank za CRDB na NMB, interest zao ziko kwenye mambo mengine kabisa - wanajihingiza kwenye Projects ambazo hawana experience yoyote nazo, Projects nyingine zinapelekwa mabonde kuinama sijuhi kuwa-please akina NANI?
 
Back
Top Bottom