CAG KUMBUKA JIPU HILI

wandamba

JF-Expert Member
Apr 29, 2014
479
1,000
*CAG KUMBUKA MAUMIVU YA JIPU UTUSAIDIE WANACHADEMA*

Jana mwanachama mwenzetu wa Chadema amefanya uamuzi mgumu.

Ni mgumu kwa tunaojua hali ilivyo ndani ya chama maana mle kuhoji masuala flani flani huwa ni issue.

Sasa mwenzetu kathubutu kamwandikia CAG afanye special audit maana Chadema inapokea fedha za umma kwa njia ya ruzuku lakini kila siku inahoji Serikali tu lakini yenyewe inatubania wanachama wake kujua yanayojiri huku chama kikiishi katika kaofisi kakujibana pale Ufipa.

Ni fursa kwa Chama sasa kuonesha uwazi kinatumiaje fedha za wananchi.Maana OGP ilipofutwa tukapiga kelele sasa tushirikiane na wakaguzi ndio uwazi wenyewe.

Na huyo mtu anaitwa CAG naye achangamke asiwe kama maofisi mengine ya umma-unaandika barua weeee hakuna majibu.

Katika hili CAG tunakutegemea sana ujue.Nakukumbusha pia maumivu ya jipu usipotekeleza haya tutamwomba mtumbuaji aje na mkasi. Haya kazi kwako.

Tusaidie kukiimarisha chama hiki kiwe imara na tuone value for money.Sio watu wanatumbua tu fedha "kufly to Kia" mara bata Nairobi mara kwenda kuzika mbwa live. Yani watu wanakula bata tu chama kikiwa hoi.

CAG kaanze hata leo.Tunataka value for money please!!!

_Niito Ole Saigoran, kada wa chama kubwa Chadema Ngorongoro_
 

jose law

Member
Oct 5, 2013
14
45
Tupe taarifa ya mapato na matumizi ya nyumbani kwako ili tupate uwazi na wewe pia
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom