CAG kapoteza mwelekeo?

Kamakabuzi

JF-Expert Member
Dec 3, 2007
2,859
1,301
Wakati JK anajibu maswali juzi, alisema Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa serikali (CAG) anaendelea na kazi ya kuhakiki madai ya walimu ili yaweze kulipwa. Nina tatizo kidogo:

-Kwa kawaida na imezoeleka kuwa CAG hufanya kazi kama mkaguzi wa nje ( external auditor), hivyo kazi yake huwa siyo kutengeneza hesabu bali kupitia hesabu zilizokwisha tengenezwa na kutoa maoni kama zinaonyesha hali halisi (to form an independent opinion on the accounts presented to him). Sasa CAG anapoanza kuhakiki madeni kabla hayajalipwa, baadae nani atakagua? Maana yake he is now playing the role of an accountant or internal auditor - nani sasa atakuwa external auditor?

- Je kama baadae ataendelea na kazi yake kama external auditor ( kama anavyofanya kwa hesabu za serikali za mitaa nk) si itaonekana amekuwa kigeugeu?
Mimi naona kuna conflict somewhere; huwezi kuverify madeni na yakishalipwa uje u-form an independent opinion juu ya madeni hayo; na kwa kweli huwezi kuja tena ukafanya ukaguzi as an independent person. Kwa vyovyote utapenda kuonyesha kuwa what you did was right!

Si vyema CAG akaanza kutumiwa na wanasiasa.

Nadhani NBAA wanaweza kutupa ufafanuzi wa suala hili.
 
Issue ya walimu inajulikana na CAG anacho hakiki ni uhalali wa baadhi ya malipo kwani ilisha ripotiwa kuwa kulikuwa na majina ya walimu bandia, na wengine wakiandikiwa malipo yasiyo halali.
 
Issue ya walimu inajulikana na CAG anacho hakiki ni uhalali wa baadhi ya malipo kwani ilisha ripotiwa kuwa kulikuwa na majina ya walimu bandia, na wengine wakiandikiwa malipo yasiyo halali.

Fine; issue hapa ni kuwa baada ya CAG kuhakiki na malipo yakafanyika, nani atakuja kufanya ukaguzi wa nje? It is about professionalism! As a professional auditor hataweza tena kukagua na kuform an independent opinion on the whole issue maana ameshakuwa part and parcel of the issue.
 
Back
Top Bottom