CAG: Hati za malipo za tzs bil. 91.3 zafichwa zisigaguliwe kwa s/kuu pekee

MZALENDOWAKWELIKWELI

JF-Expert Member
Feb 5, 2012
330
210
Thamani ya Hati za Malipo (Vocha) alizoziomba kuzikagua akanyimwa bila maelezo yanayoeleweka zimepaa kutoka TZS Milioni 361.79 kwa mwaka wa fedha 2014/2015 hadi kufikia TZS Bilioni 91.347 kwa mwaka wa fedha 2015/2016.....

Nanukuu "Nilitoa wito kwa Menejimenti za Taasisi husika kuziwasilisha hati za malipo zilizokosekana kwa ajili ya ukaguzi, ambapo
kushindwa kufanya hivyo, hatua stahiki lazima zichukuliwe kwa mujibu wa Sheria ya Fedha za Umma na Kanuni zake kutokana na kutangaza kupatikana kwa hasara inayofikia shilingi 91,347,958,833"

Kwa mujibu wa ripoti hiyo Sura ya 10 CAG anabainisha kuwa Kukosekana kwa hati za malipo na viambatisho vyake, kulisababisha kutoweza kubaini uhalali, uhalisia, aina na madhumuni ya matumizi hayo ya kiasi cha Shilingi 91,347,958,833 ambacho Kwa mujibu wa Kanuni ya 18(1)(f) & (2) ya PFR, 2001 kukosekana kwa hati hizo za malipo kinataja kitendo hicho ni sawa na hasara ya upotevu wa fedha.

Kwa mujibu wa kanuni hizo za fedha itampasa Mhasibu Mkuu wa Serikali kuorodhesha malipo hayo kwenye Taarifa ya Hasara ya mwaka
ili yachunguzwe kwa kina na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali.

Aidha CAG ktk ripoti hiyo anashauri...."hatua za kufidia hasara hiyo lazima zichukuliwe kwa mujibu wa Kanuni 24 ya Kanuni za Fedha, 2001 kutoka kwa maafisa waliohusika kusababisha "

Kuisoma Ripoti hiyo ya Ukaguzi wa Serikali Kuu bofya hapa http://www.nao.go.tz/?wpfb_dl=216

Kusoma Ripoti ZOTE za CAG zikiwemo Serikali za Mitaa/Mashirika/Ripoti za Ufanisi bofya

National Audit Office of Tanzania » Mwaka wa Fedha 2015/16
 
Duh!!
Hizo zingetosha kuweka lami ya Mbeya-makete - ikonda.
Ela zote zikiingia kwenye kujenga barabara mtaani hakutakalika... Ndo haya tunayaona sasa hivi kila mtu analalamika ukata.. Mwisho wa sku hzo ela zjngerudi huko huko mtaani na kupunguza njaa
 
Back
Top Bottom