CAG bora wa muda wote nchini Tanzania

CAG bora wa muda wote nchini Tanzania

Milima ya Uluguru

New Member
Joined
Nov 3, 2019
Posts
2
Reaction score
3
CAG BORA WA MUDA WOTE NCHINI TANZANIA.

Leo 13:15pm,07/04/2019.

Huyu ndiye CAG bora wa muda wote nchini Tanzania ambaye aliibua madudu na kuzifanya taasisi za Umma kushughulikia ufisadi na kuanza kuuchukia kwa dhati ufisadi.Huyu ndiye aliyewapa kiki Chadema kwa "Special Audit" zake ambazo Chadema walizibeba kama ajenda zao.

He did it professionally,hakuwahi kuichukiza taasisi yoyote na hakuwahi kuchukiwa na taasisi au mtu yoyote zaidi aliheshimika sana hata leo baada ya kustaafu anaheshimika sana, ndiye "measuring stick" katika kufanya kazi hiyo kwa weledi,hekima na busara.

Nimewahi kusoma kitabu cha Ludovic Uttoh cha kalamu isiyo na wino nilielewa hekima na busara aliyotumia kufikisha ujumbe bila kuudhi mtu au taasisi kwa kuita "dhaifu".

Uttoh alijipatia umaarufu wa Special Audit nyingi alizofanya ambazo chanzo chake ni kuibuka kashfa mbalimbali bungeni na kupewa jukumu la kwenda kufanya "Special Audit". Lakini pia akirejea aliyoyataja wakati wa Statutory Audit zake.

Mfano wa Special Audit zilizompa umaarufu Uttoh ni pamoja na EPA, Escrow Tegeta Account, Rushwa ya Jairo na kashfa ya Ujenzi wa Bandari.

Uttoh aliaminiwa kwa shughuli nyeti za kuikagua Serikali katika Statutory Audit zake na hata alipoombwa kufanya Special Audit kwa kashfa zilizoibuka bungeni alifanya kazi hiyo kwa weledi mkubwa, hekima na busara,kwa utaalamu wake aliona mengi, kwa kuwa alikuwa mkomavu wa Uongozi, aliandika report na kuikabidhi kunakohusika na kusubiria bunge kuja kujadili na kama bunge lilijadili na kuonekana haja ya kufanya Special Audit basi alienda kufanya Special Audit kwa mahala palipoleta utata,hekima yake ilimtuma kutosambaza umbea kama taaluma yake inavyomtaka kuwa mweledi hata kama fursa ya kusambaza umbea ilipatikana.

Kwa maadili ya Utumishi wa Umma na maadili ya taaluma ya Uhasibu hutakiwi kuongelea ulichokikagua kama bado hakijawa hadharani kupitia yule aliyekutuma kufanya Ukaguzi,kwa kuongelea kitu ulichokiandikia report kabla ya aliyekutuma kukiweka hadharani ili kifanyiwe kazi,ni sawa na kwenda “mtaani” na kuanika yaliyo chumbani au ndani ya nyumba ambayo mnalala na na kusababisha wengine wajue kwamba hamfungagi mlango kwa kuwa komeo limevunjika,kiutumishi wa Umma ni kuvunja miiko ya kimaadili na ni makosa makubwa ambayo inatakiwa mhusika afukuzwe katika Utumishi,awe "fired". Kwa CAG ambaye analindwa kikatiba na sheria zaweza kumfanya awe hana hatia, ila morally he does not fit to head a public office any more.He should be fired.CAG atakuwa ametenda kosa la kuvunja miiko ya kimaadili.

Administratively, CAG anawajibika kwa taasisi ya Utawala (Executive Branch) na ndiyo maana mara baada ya kuandaa report, hufika Ikulu na kuiwasilisha. Basically CAG anachaguliwa na Rais wa Nchi ambae ndiye kiongozi wa "Executive Branch". Baada ya hapo,CAG hutakiwa kwenda bungeni kuiwasilisha mbele ya bunge. Sasa basi kwa muktadha huo, anapowasilisha report mbele ya Rais… “it goes without saying, kwa maana Mh Rais ndiye boss wake” anapowasilisha tena report bungeni “it is simple understanding, Spika ambae ni mkuu wa taasisi ya Bunge anakuwa ndiye boss wa CAG kwa wakati huo”

-Huu ni msumari wa moto kwa chadema.

Wakati wa Uzinduzi wa kitabu chake cha Uwajibikaji ndani ya Kalamu isiyokuwa na Wino,alipohojiwa na Waandishi wa habari alitoa maneno haya,nanukuu..

"Namsifu na kumpongeza sana Mh Rais Dk. John Pombe Magufuli, Serikali anayoiongoza imekuwa ikitekeleza mapendekezo ambayo niliyatoa wakati nikiwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kabla ya kustaafu kwangu mwaka 2014"

Utouh alisema udhibiti mbovu uliokuwa ukiikosesha Serikali mapato na kuisababishia hasara, umefanyiwa kazi. Alitolea mifano ya changamoto za: watumishi feki pamoja na mita za mafuta bandarini (TPA) zilizokuwa hazitumiki.

"Katika kipindi cha miaka mitatu, suala la uwajibikaji kwa watumishi wa Serikali na ulinzi wa rasilimali za umma ni mkubwa sana.Nampongeza sana Mh Rais Dk. John Pombe Magufuli."

-Uwajibikaji Ndani ya Kalamu Isiyokuwa na Wino "Accountability in an Inkless Pen".

-Kwenye kitabu cha Uwajibikaji ndani ya kalamu isiyokuwa na Wino,Utouh amezungumzia uhusiano baina ya Ofisi ya Taifa ya ukaguzi wa hesabu za Serikali na serikali yenyewe kupitia Ofisi ya Katibu Mkuu. Kwa mujibu wa sheria ripoti za Mkaguzi wa Serikali zinatakiwa kukabithiwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano kabla ya tarehe 31 mwezi Machi kila mwaka. Ieleweke kuwa ripoti za CAG zimejikita katika ukaguzi wa hali za kifedha katika Serikali

Aidha, kitabu kinaelezea ukaguzi maalum uliofanyika juu ya 'External Payment Arrears (EPA)' ambapo serikali iliweza kugundua kuwa zaidi ya TZS 60 billion kati ya TZS 90 billion zilithibitika kuibiwa kutoka Benki Kuu ya Tanzania. Zaidi ya hiyo, kitabu kimeweza kuorodhesha mambo muhimu ambayo yalifanyiwa ukukaguzi wakati Utouh alipokuwa Mkaguzi Mkuu na Mthibiti wa hesabu za Serikali. Mambo hayo ni pamoja na Escrow, PRIDE and UDA.

-Kwa nini Ludovick Utouh aliandika kitabu.

Licha ya kupewa kinga kubwa na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pengine kuliko mtu mwingine yeyote, lakini bado CAG alikutana na changamoto nyingi katika Utendaji wake wa kazi,Wakati mwingine CAG Ludovick Utouh alikuwa akijiona yuko mwenyewe kwa sababu anakuja na pendekezo ambalo anaamini ndani ya moyo wake kuwa likitelekezwa litaisaidia Serikali, halafu halitekelezwi.hiyo ndiyo sababu iliyomfanya aandike kitabu.

“Ni sababu hiyo ikanifanya niandike hiki kitabu ili kuelimisha kuhusu dhana ya uwajibikaji na kuwakumbusha Watanzania wenzangu kuwa hili suala ni letu sote. Najua fedha na nguvu niliyotumia kuandika kitabu hiki haitarudi kwa sababu Watanzania hawana utamaduni wa kusoma, ila binafsi nimesukumwa niandike kutoa elimu.”

Utoah alisema mambo kadhaa alikuwa akishauri, lakini hayakufanyiwa kazi hadi Serikali ya Awamu ya Tano ilipoingia madarakani na kuyaangalia kwa jicho la tatu.

Aliyataja baadhi ya mambo hayo kuwa ni pamoja na sakata la watumishi hewa, Escrow, kutambulika kwa makao makuu ya Serikali na mgogoro wa kimasilahi unaotokana na wabunge kuingia kwenye bodi za mashirika ya umma.

Kuhusu suala la watumishi hewa, alisema kwa muda mrefu alikuwa akilitolea ushauri, lakini haukizingatiwa ila sasa baada ya hatua kuchukuliwa manufaa yameonekana kutokana na fedha nyingi kuokolewa.

-Furaha ya Ludovick Utoah,ni kufanyiwa kazi kwa Ushauri wake,katika Serikali ya Awamu hii ya tano.

Majawabu chanya ya Serikali kufanyia kazi ushauri wa aliyekuwa CAG, Ndugu Ludovick Utouh umeleta tija kwa Serikali baada kuokoa fedha nyingi zilizokua zinaliwa na watu wachache.

Fedha hizo zilizookolewa ndio zinatumika katika mpango wa kutoa elimu bure takribani Billion 20 kila mwezi,kuongeza mitandao ya huduma za maji na umeme mijini na vijijini, kuzipa Halmashauri 67 Shillingi Billion moja na nusu kwa ajili ya kujenga Hospitali za Wilaya, kuongeza bajeti ya dawa na vifaa tiba ,kujenga vituo vya afya na Zahanati, kuboresha kilimo, kujenga miundombinu ya Barabara na kadhalika.

Tanzania ni nchi tajiri sana na ndio maana Serikali inaendelea kujenga miradi mikubwa ya reli ya kisasa Standard Gauge,mradi mkubwa wa kufua umeme katika Bonde la Mto Rufiji (Stiegelers Gorge) ,ununuzi wa ndege mpya kabisa kwa ajili ya shirika letu la kizalendo la Air Tanzania (ATCL) bila ya wasiwasi wowote.

Rais Magufuli ni kiongozi mwenye maono mapana sana ,anataka nchi hii iingie katika orodha ya mataifa yenye nguvu kubwa kiuchumi Barani Afrika na Duniani ,Nchi itakayokua na uwezo wa kutoa misaada kwa nchi nyingine (Donor Country) na ndio maana anadhibiti upotevu wa mapato katika madini,utalii, gesi,bandarini,uvuvi pamoja na kutoa msukumo katika ujenzi wa viwanda nchi nzima.

Nimalizie kwa kumshukuru Ndugu Ludovick Utouh kwa Utumishi wake uliotukuka katika Serikali, nimshukuru kwa hekima na busara aliyokuwa nayo, na nitoe rai kwa Watumishi kuiga weledi, maadili na Utumishi bora aliouonyesha katika kipindi chake cha Utumishi, hata miaka yake nane ya Utumishi kama CAG. ahsante Mwenyezi Mungu kwa kuibariki Tanzania, tupe neema ya kutumia vyema baraka zako ulizotujaalia.

Nikiishia hapa, Mimi ni,
Msemakweli Chakubanga.
Dar es Salaam.
0755078854.
 
Huu ndio ufafanuzi wa profesa Shivji

1572854174302.png
 
Angefanya kazi na jiwe ndo ungekuwa na jeuri ya kumpamba au la.
 
CAG Utouh wasn't the best we had. Assad was and shall remain the best CAG ever for a long time to come. Utouh alijinyenyekesha kwa watawala hivyo kushindwa kuusimamia wajibu wake wa kuita spade a spade.
 
Kwenye utawala wa jiwe naye angepata msukosuko mkubwa. Hasa pale kwenye 1.5 mil
 
Back
Top Bottom