CAG apanga 'kuua' warsha serikalini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CAG apanga 'kuua' warsha serikalini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Informer, Sep 16, 2012.

 1. Informer

  Informer JF-Expert Member

  #1
  Sep 16, 2012
  Joined: Jul 29, 2006
  Messages: 1,223
  Likes Received: 2,434
  Trophy Points: 280
  Imeandikwa na Halima Mlacha | HabariLeo | Sept 14, 2012


  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), Ludovick Utouh amesema ameishauri Serikali kudhibiti warsha za mara kwa mara na zitakazokubalika ziwe na mitihani ambayo matokeo yake watapewa mabosi wa watahiniwa.

  Akizungumza katika semina ya waandishi wa habari kuhusu namna ya kuripoti masuala ya rushwa kutokana na ripoti za CAG, Utouh alisema tayari mfumo huo umeanza katika Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali.

  Kwa mujibu wa Utouh, katika kila warsha hasa zinazozidi siku tano, washiriki wa warsha hizo watapaswa kufanya mtihani na matokeo ya mtihani kuhusu mada zilizojadiliwa, yatapelekwa kwa mabosi wa washiriki.

  Alifafanua kuwa, mabosi hao watatakiwa kutumia matokeo hayo katika kupandisha vyeo watumishi walioshiriki katika semina hizo au vinginevyo.

  Alisema katika ofisi yake ya NAOT wameanza kutumia mfumo huo ambapo warsha zote zinazozidi siku tano, washiriki hulazimika kupewa mitihani na matokeo ya mtihani huo huwasilishwa kwake.

  "Sisi tumeanza mfumo huu ambao unasaidia kutambua value for money,(thamani halisi) warsha yoyote inayozidi siku tano, washiriki hupewa mtihani na matokeo yao yaliyowasilishwa kwangu huyatumia kuwapromoti au kuwaadhibu," alisema.

  Alikuwa akijibu swali la mmoja wa washiriki wa warsha iliyoandaliwa na ofisi yake ambaye alitaka kujua hatua zilizochukuliwa na NAOT katika kudhibiti warsha za mara kwa mara za taasisi za Serikali zisizo na tija.

  Pamoja na hayo Utouh alibainisha wazi kuwa ofisi yake imekuwa ikifanyakazi kwa uhuru wa kutosha hasa ikilinganishwa na ofisi nyingine zinazofanyakazi kama hiyo ya ukaguzi duniani.

  "Na hii ni kutokana na ukweli wa Sheria iliyotumika kuanzisha NAOT ambayo inabainisha wazi kuwa ni kosa kama mtu au taasisi isipotoa ushirikiano wa kutupatia taarifa tunazozohitaji katika ukaguzi wetu," alisema.

  Lakini pia kutokana na uwezo na taaluma za wafanyakazi wa ofisi hiyo ya CAG, wamekuwa wakiaminika ndani na nje ya nchi ambapo hivi karibuni walifanya ukaguzi wa hesabu za Umoja wa Mataifa (UN) na Shirika la Maendeleo la UN (UNDP) ambalo hesabu zake ni kubwa zaidi ya bajeti ya Tanzania.

  Akizungumzia suala la magari ya gharama kubwa yanayotumiwa na Serikali, Utouh alisema moja ya kazi ya ofisi ni pamoja na kutoa ushauri kwa Serikali kuhusu namna ya kupunguza na kudhibiti matumizi ya fedha za Serikali.

  Alisema NAOT imekuwa ikiishauri Serikali kwa muda mrefu katika manunuzi yake ya magari ya Serikali kuzingatia ununuzi wa magari yenye gharama nafuu jambo ambalo kwa sasa limeanza kuzaa matunda.

  "Tulishawahi kukagua ununuzi wa magari na kubaini kuwa magari mengi ya Serikali yanayonunuliwa ni ya gharama kubwa na yanatumia mafuta mengi, tukaishauri Serikali kuwa magari ya aina hii si ya lazima," alisema.

  Aliongeza "Tuliwahoji, je kiongozi akiwa jijini Dar es Salaam anahitaji VX kutoka Mikocheni hadi katikati ya jiji? Suala la warsha za mara kwa mara limekuwa likipigiwa kelele hadi kufikia Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuingilia kati na kupiga marufuku warsha na semina zisizo na tija.
   
 2. i

  iMind JF-Expert Member

  #2
  Sep 16, 2012
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 1,907
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  CAG aliyasema haya akiwa kwenye warsha. Mwandishi wa habari aliandika habari hii akiwa kwenye warsha. Nina wasi wasi CAG anataka kugombea cheo cha kisiasa 2015
   
 3. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #3
  Sep 16, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  ni vema kwani wengine wanasign na kuchukua hela jioni bila hata kuhudhuria
  wau wengine hutumia warsha kuchati facebbok na kusoma email jioni anakamata mshiko
  ukimuuliza kaelewa nini anatoka mtupu.
  itapunguza pia warsha za kijinga na za kujitajirisha huko serikalini, big up CAG
   
 4. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #4
  Sep 16, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Jamani, MIMI NI BOSI NIFANYE MTIHANI? kuliko kwanza nipate hicho kiinua MGONGO [per DM ya tumbo langu kwanza] Si Wengi tutafeli ?

  Warsha nyingi ni sisi kula sasa hii ya testi tena itatumaliza; Itanifanya nitafute mpango Mwingine wa KULA...
   
 5. Tram Almasi

  Tram Almasi JF-Expert Member

  #5
  Sep 16, 2012
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 755
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mtihani? Hapo mambo yatakuwa magumu ss. Wenye kuzunguka TZ kuhudhuria kila kukicha,sasa naona kbs watazikacha.
   
 6. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #6
  Sep 16, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Nina wasiwasi na hii technique ya CAG kama itazaa matunda. Ukweli ni kwamba, watumishi wa umma wanatumia hizi washa kama namna ya kujiongezea kipato, kwani mishaara yao ni midogo... Kama KWELI wakiwabana kwenye hizi warsha na semina, kwa hakika Serikalini watabaki wale watumishi waliosoma kwa kuungaunga (kama Lukuvi), lakini sio competent individuals...
   
 7. Uliza_Bei

  Uliza_Bei JF-Expert Member

  #7
  Sep 16, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 3,109
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  wazee vilaza wanaisha sisi kama ni mitihani tunazitaka warsha za kutosha japo nasi tule maana ufisadi hatumo
   
 8. m

  mpigauzi JF-Expert Member

  #8
  Sep 16, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Anaweza? Tusubiri. Kwani hata PM alishawahi kusema hilo lakini no implementation
   
Loading...