Mpaka sasa najiuliza kwa nini Spika alikuwa anakwamisha kwa maksudi kuanikwa kwa wizi huu
Katika ripoti ya CAG umeibuliwa ufundo wa hatari
Hasara katika Kununua Ardhi ya Sh. Bilion 4.17
CAG anasema..........Mfuko wa NSSF uliingia mikataba tarehe 16 Septemba 2010 na 12 Oktoba 2010 wa kununua ekari 277 (Muuzaji wa kwanza) na ekari 180 (Muuzaji wa pili) eneo la Kiluvya kwa Sh. bilioni 3.32 na Sh. bilioni 1.62, mtawalia. Kufuatia mapitio ya taarifa ya tathmini ya ekari 277 nilibaini kuwa thamani ya ardhi hiyo kwa
kipindi cha mwezi Oktoba 2010 ilikuwa Sh. milioni 416.40;
wakati makadirio ya thamani ya soko kwa ekari 180 ilikuwa Sh.milioni 720. Kwa hiyo, gharama ya ardhi iliyonunuliwa ilizidishwa kwa kiasi cha Sh. bilioni 2.90 na Sh. milioni 900 mtawalia na hivyo, kusababisha jumla ya hasara kuwa Sh.bilioni 3.80. Nilibaini pia kuwa, muuzaji wa kwanza aliripoti
mauzo yake kwa TRA kwa Sh. milioni 900 badala ya Sh. bilioni
3.32, kwa sababu hiyo kodi (stamp duty) ya Sh. milioni 24.24
haikulipwa.
Zaidi ya hayo, nilibaini hasara nyingine ya Sh. milioni 370
iliyotokana na NSSF kununua ekari 67.4 kwa muuzaji bandia
eneo la Nunge, Bagamoyo. Mahakama ya wilaya katika shauri
la madai shauri Na. 7 la 2003 na Mahakama Kuu katika Rufani
ya Madai ya shauri Na. 7 la 2006 ilibaini kwamba, muuzaji
hakuwa mmiliki wa ardhi ambayo iliuzwa kwa NSSF. Kwa
ujumla, NSSF ilipata hasara ya Sh. bilioni 4.17 katika kununua
ardhi na ililipa kiasi kidogo cha kodi (stamp duty) kwa Sh.
milioni 24.24.
Ninapendekeza kuwa Bodi ya Mfuko na Menejimenti ichukue
hatua stahiki kwa wale waliohusika katika mchakato mzima wa kununua ardhi iliyosababisha hasara hiyo ya Sh. bilioni 4.17
Watumishi kugawiwa mabilioni kununua hisa vodacom bila riba wala mikataba
CAG anasema..............
Mfuko ulitoa mkopo bila riba wa Sh. bilioni 1.65 kwa watumishi
na Sh. milioni 206 kwa wachangiaji (Members) wengine ili kununua hisa za Vodacom. Hata hivyo, hakukuwa na mikataba kati ya Mfuko na wanufaika hao. Pia, namna ya urejeshwaji wa mikopo iliyotolewa kwa wachangiaji wengine imebaki kuwa
mashakani. Mkopo uliotolewa kwa wachangiaji wengine
ulikuwa kinyume na mafao yaliyoelezwa katika sehemu ya
Sheria ya Pesheni ya NSSF ya mwaka 2015.
Kukosekana kwa mikataba kwa fedha zilizolipwa kwa ununuzi
wa hisa za Vodacom kati ya Mfuko na wanufaika wa mkopo
kunaweka mazingira ya wakopaji kutokurejesha mikopo hiyo.
Hakika nchi hii inaliwa.