Kipenzi Changu
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 58,041
- 134,315
Mpaka sasa najiuliza kwa nini Spika alikuwa anakwamisha kwa maksudi kuanikwa kwa wizi huu
Katika ripoti ya CAG umeibuliwa ufundo wa hatari
Hasara katika Kununua Ardhi ya Sh. Bilion 4.17
CAG anasema......
Mfuko wa NSSF uliingia mikataba tarehe 16 Septemba 2010 na 12 Oktoba 2010 wa kununua ekari 277 (Muuzaji wa kwanza) na ekari 180 (Muuzaji wa pili) eneo la Kiluvya kwa Sh. bilioni 3.32 na Sh. bilioni 1.62, mtawalia. Kufuatia mapitio ya taarifa ya tathmini ya ekari 277 nilibaini kuwa thamani ya ardhi hiyo kwa kipindi cha mwezi Oktoba 2010 ilikuwa Sh. milioni 416.40; wakati makadirio ya thamani ya soko kwa ekari 180 ilikuwa Sh.milioni 720. Kwa hiyo, gharama ya ardhi iliyonunuliwa ilizidishwa kwa kiasi cha Sh. bilioni 2.90 na Sh. milioni 900 mtawalia na hivyo, kusababisha jumla ya hasara kuwa Sh.bilioni 3.80.
Nilibaini pia kuwa, muuzaji wa kwanza aliripoti mauzo yake kwa TRA kwa Sh. milioni 900 badala ya Sh. bilioni 3.32, kwa sababu hiyo kodi (stamp duty) ya Sh. milioni 24.24 haikulipwa.
Zaidi ya hayo, nilibaini hasara nyingine ya Sh. milioni 370 iliyotokana na NSSF kununua ekari 67.4 kwa muuzaji bandia eneo la Nunge, Bagamoyo. Mahakama ya wilaya katika shauri la madai shauri Na. 7 la 2003 na Mahakama Kuu katika Rufani ya Madai ya shauri Na. 7 la 2006 ilibaini kwamba, muuzaji hakuwa mmiliki wa ardhi ambayo iliuzwa kwa NSSF.
Kwa ujumla, NSSF ilipata hasara ya Sh. bilioni 4.17 katika kununua ardhi na ililipa kiasi kidogo cha kodi (stamp duty) kwa Sh. milioni 24.24.
Ninapendekeza kuwa Bodi ya Mfuko na Menejimenti ichukue hatua stahiki kwa wale waliohusika katika mchakato mzima wa kununua ardhi iliyosababisha hasara hiyo ya Sh. bilioni 4.17
Watumishi kugawiwa mabilioni kununua hisa Vodacom bila riba wala mikataba
CAG anasema....
Mfuko ulitoa mkopo bila riba wa Sh. bilioni 1.65 kwa watumishi na Sh. milioni 206 kwa wachangiaji (Members) wengine ili kununua hisa za Vodacom. Hata hivyo, hakukuwa na mikataba kati ya Mfuko na wanufaika hao. Pia, namna ya urejeshwaji wa mikopo iliyotolewa kwa wachangiaji wengine imebaki kuwa mashakani.
Mkopo uliotolewa kwa wachangiaji wengine ulikuwa kinyume na mafao yaliyoelezwa katika sehemu ya Sheria ya Pesheni ya NSSF ya mwaka 2015.
Kukosekana kwa mikataba kwa fedha zilizolipwa kwa ununuzi wa hisa za Vodacom kati ya Mfuko na wanufaika wa mkopo kunaweka mazingira ya wakopaji kutokurejesha mikopo hiyo.
Hakika nchi hii inaliwa.