C.I.F ni nini?

kupe

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
1,032
1,500
Kuna gari nimeagiza toka japan aina ya pajero ya mwaka 2004 yenye cc 1300 . na gharama zote nilizolipa hadi kufika dar ni dola 3500. JE NITAILIPIA USHURU KIASI GANI plus na clearing agent. Tafadhari anayefahamu.
 

Soki

JF-Expert Member
Jan 5, 2011
1,304
1,195
Kama sijakosea, chukua hiyo 3,500 ambayo ndo CIF + 25% = y.
Hiyo y ongeza 18% ndo kiasi utakacholipa.

Lakini kuna aina za magari unaongeza TENA 5% ya CIF

utaongeza pia hela ya wakala wa ku clear gari lako. Pia utaongeza port charges

Nimekupa tuu picha fulani, inaweza isiwe sahihi sana lakini haitokuwa tofauti sana na hesabu hii nlokupa.

KAMA KUNA MAWAKALA WA KU CLEAR MAGARI HAPA, WANAWEZA KUKUELEZEA VIZURI ZAIDI
 

kupe

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
1,032
1,500
Mkuu soki hebu naomba nipigie hiyo hesabu unipe figure. Mimi sijaielewa.
 

mkonomtupu

JF-Expert Member
Jul 5, 2011
441
250
Gari ya cc 1300 ya mwaka 2004 mchanganuo wake ni Kama ifuatavyo
CIF*25% = import duty
3500 * 25% = 875
CIF * 5% = excise duty
3500 * 5% = 175
CIF * 18% = VAT
3500 * 18% = 630
maana yake utalipa
875+175+630 = 1680 usd + clearing charges ni maelewano.
Nina mdogo wangu anafanya kazi hizo Kama utahitaji nikuunganishe nae mpatane na mkubaliane ukiwa tayari nistue tu.
 

shizukan

JF-Expert Member
Jan 16, 2011
1,158
0
C.I.F maana yake ni Cost Insurance & Freight. Ni international commercial term ikimaanisha kuwa ndani ya bei ya bidhaa, imejumuishwa pia gharama Bima na Usafiri. Hii ina maana kuwa ukilipa hiyo C.I.F price, muuzaji anawajibika kulifikisha gari hilo bandarini na kulipakua kabisa, na wewe utawajibika kufanya clearance bandarini ikijumuisha customs duty n.k
 

Big Baba

JF-Expert Member
Oct 19, 2012
251
195
C.I.F maana yake ni Cost Insurance & Freight. Ni international commercial term ikimaanisha kuwa ndani ya bei ya bidhaa, imejumuishwa pia gharama Bima na Usafiri. Hii ina maana kuwa ukilipa hiyo C.I.F price, muuzaji anawajibika kulifikisha gari hilo bandarini na kulipakua kabisa, na wewe utawajibika kufanya clearance bandarini ikijumuisha customs duty n.k

mia ya mia mkuu
 

silent lion

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
806
1,000
mkuu kwa ufupi ushuru wake ni kama 3040000. Nikifika ofisini kesho ntakupa uhakika kuna program yao inaitwa ASYCUDA++ nitaingiza hizo detail zako ntakupa jibu. Ila nsaidie kitu kimoja. hiyo Pajero ni model gani? Pajero Mini, Pajero GDI au Intercooler
 

silent lion

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
806
1,000
mkuu kwa ufupi ushuru wake ni kama 3040000. Nikifika ofisini kesho ntakupa uhakika kuna program yao inaitwa ASYCUDA++ nitaingiza hizo detail zako ntakupa jibu. Ila nsaidie kitu kimoja. hiyo Pajero ni model gani? Pajero Mini, Pajero GDI au Intercooler?
 

asrams

JF-Expert Member
Sep 4, 2011
4,801
2,000
God bless JF leo nimejifunza kitu kipya kabisaa! Shukran wadau.


Sent from my Nokia 8310 using Tapatalk
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom